-
Iran yakosoa tuhuma zisizo na msingi za Uingereza
Oct 09, 2024 10:29Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amejibu madai ya afisa wa usalama wa Uingereza akisema: Maafisa wa serikali ya London wanapaswa kutumia ushawishi wao kusimamisha uchokozi na jinai za utawala ghasibu wa Israel badala ya kutoa tuhuma zisizo na msingi na mijadala ya kupotosha.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Wazayuni wanataka kuathiri uchaguzi wa Marekani
Oct 09, 2024 03:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni unataka kupanua vita katika eneo la Magharibi mwa Asia lengo likiwa ni kuathiri matokeo ya uchaguzi ujao wa Marekani.
-
Rais wa Iran: Ulimwengu wa watoto haupaswi kuchafuliwa na vita na uwaniaji madaraka wa watu wazima
Oct 09, 2024 03:24Rais wa Iran ameeleza kuwa ulimwengu mzuri, wa kuvutia na wa watoto wadogo wasio na hatia haupaswi kuchafuliwa na vita na uwaniaji madaraka wa watu wazima.
-
Rais wa Iran akosoa uungaji mkono wa US, EU kwa jinai za Israel
Oct 08, 2024 08:30Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezikosoa vikali Marekani na nchi za Ulaya kwa kuunga mkono jinai zinazofanywa na utawala khabithi wa Israel.
-
Araghchi: Iran itajibu vikali chokochoko zozote za utawala wa Kizayuni
Oct 08, 2024 02:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa Tehran haina nia ya kushadidisha mivutano wala kuzusha vita katika eneo hili lakini wakati huo huo iko imara na tayari kutoa majibu makali zaidi iwapo utawala wa Kizayuni utafanya chokochoko zozote dhidi yake.
-
Iran yaionya Israel, yasisitiza ‘haitarudi nyuma kamwe’ kuhusu haki zake
Oct 08, 2024 00:10Msemaji wa serikali ya Iran, Fatemeh Mohajerani, amesema Iran kamwe haitarudi nyuma katika kutetea maslahi yake ya kitaifa huku akiuonya utawala wa Kizayuni wa Israel usithubutu kuvuka mipaka.
-
Yajue makombora ambayo Iran iliyatumia katika ‘Operesheni ya Ahadi ya Kweli II’ dhidi ya Israel
Oct 07, 2024 13:43Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huangazia baadhi ya mafanikio katika uga wa sayansi, tiba na teknolojia nchini Iran na leo tutaangazia mafanikio ya Iran katika uga wa ulinzi.
-
Wanachuoni 3,000 wa Kisuni wamwandikia barua ya shukrani Kiongozi Muadhamu
Oct 07, 2024 07:33Wanachuoni 3,000 wa Kisuni wa nchini Iran wamemwandikia barua ya shukrani Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wakimshukuru na kumpongeza kwa operesheni ya Ahadi ya Kweli II iliyoutia adabu utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais Pezeshkian: Iran inakaribisha mazungumzo na Ulaya ili kuimarisha uhusiano
Oct 07, 2024 03:54Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili linakaribisha mazungumzo na nchi za Ulaya kwa ajili ya kutatua masuala na kuimarisha uhusiano.
-
Iran yanakusha madai ya kuvuruga usalama katika Bahari Nyekundu
Oct 06, 2024 22:51Mwakilishi wa Iran katika Kamati ya Ulinzi wa Mazingira ya Baharini (MEPC) amekadhibisha madai yaliyotolewa na Marekani dhidi ya Iran kuhusu usalama wa Bahari Nyekundu.