-
Mazuwwar milioni 2 kutoka Iran waelekea Iraq kwa ajili ya Arubaini ya Imam Hussein (as)
Aug 19, 2024 08:22Halmashauri ya Usafiri nchini Iran imetangaza kuwa kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 17 Agosti, Mazuwwar wapatao 2,055,396 walipitia katika vivuko vya mpaka wa Iran na kuingia Iraq ili kushiriki katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as).
-
Iran: Serikali, mataifa na mashirika yote yawajibike kuhusu maafa ya Gaza
Aug 19, 2024 08:18Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa serikali na mataifa yote na mashirika ya kimataifa yanapaswa kuwajibika kuhusu maafa ya kutisha yanayoendelea hivi sasa katika Ukanda wa Gaza, na iwapo hayatachukua hatua, basi yatalaaniwa milele na kustahili kulaumiwa katika mahakama ya historia na dhamiri ya binadamu.
-
Iran: Jamhuri ya Kiislamu ni utawala imara wenye nguvu za kieneo na kimataifa
Aug 19, 2024 02:40Ubalozi wa Iran mjini London umesema kuwa, pamoja na kwamba mwaka 1953, Marekani na Uingereza zilifanya mapinduzi dhidi ya serikali ya wakati huo ya Iran lakini hivi sasa Jamhuri ya Kiislamu ni utawala imara na wenye nguvu kubwa za kieneo na kimataifa.
-
Mchakato wa upigaji kura katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ili kuidhinisha baraza la mawaziri
Aug 18, 2024 09:49Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) inaendelea na vikao vya kujadili sifa waliopendekezwa kuwa mawaziri katika serikali ya awamu 14 kabla ya kupigiwa kura.
-
Iran: Baka la aibu la Mapinduzi ya kijeshi ya 1953 litabakia milele kwenye mapaji ya nyuso za US na UK
Aug 18, 2024 08:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, baka la aibu la kuiondoa madarakani Serikali halali ya Iran iliyochaguliwa na wananchi, kupitia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 28 Mordad 1332 (Agosti 19, 1953) na la kuuhami Udikteta kisiasa, kiusalama na kijeshi litaendelea kubakia milele kwenye mapaji ya nyuso za tawala za Marekani na Uingereza.
-
Iran: Tuna haki ya kujibu mapigo ya mauaji ya kigaidi ya Haniyah
Aug 17, 2024 23:29Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ina haki ya kujibu kwa njia halali kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumuua kigaidi Ismail Haniyah, aliyekuwa Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas akiwa ziarani hapa mjini Tehran.
-
Putin amwalika Pezeshkian katika mkutano wa BRICS
Aug 17, 2024 23:00Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow, Russia, amesema kuwa Rais Vladimir Putin wa Russia amemwalika Rais Masoud Pezeshkian kushiriki katika mkutano wa wakuu wa kundi la BRICS.
-
Rais Pezeshkian asisitiza kuchungwa misingi ya heshima, hekima na maslahi ya Iran katika uga wa kimataifa
Aug 17, 2024 07:32Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kupanga na kuratibu uhusiano wa kimataifa kwa kuzingatia misingi ya heshima, hekima na maslahi ni miongoni mwa majukumu yanayofanyiwa kazi na serikali ya 14 ya Iran.
-
Aboutorabi Fard: Wazayuni lazima tutawatia adabu
Aug 16, 2024 08:21Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, kutiwa adabu utawala wa Kizayuni ni jambo lisiloepukika na watu wote wanaelewa vyema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitoziacha jinai hizo zipite hivi hivi.
-
"Mateka wa vita wa Iran ni nembo ya Muqawama dhidi ya adui"
Aug 16, 2024 07:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Mafungwa wa Vita ni nembo ya Muqawama na kusimama kidete taifa kubwa la Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya ubeberu na utwishaji wa maadui wa taifa hili.