-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran apongeza nafasi ya kipekee ya Shahidi Nasrullah
Oct 11, 2024 07:47Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuuawa shahidi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah kinyume na ulivyotarajiwa utawala wa Kizayuni wa Israel, kumeutia moyo na kuupa ari kubwa mhimili wa Muqawama katika eneo.
-
Spika: Mauaji ya kigaidi kuharakisha kuporomoka utawala wa Kizayuni
Oct 11, 2024 07:02Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, mashambulizi ya anga na mauaji ya kigaidi yanayofanywa na utawala haramu wa Israel hayatakuwa na matokeo mengine isipokuwa kuharakisha kusambaratika na kuangamia kwa utawala huo wa Kizayuni.
-
Iran: Tumejiweka tayari kikamilifu kulinda mamlaka ya utawala ya ardhi yetu
Oct 11, 2024 04:16Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imejiweka tayari kikamilifu kulinda mamlaka yake na umoja wa ardhi yake dhidi ya uvamizi na uchokozi wowote utakaoyalenga maslahi yake makuu na usalama wake.
-
The Telegraph: Iran imethibitisha uwezo wake wa kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani
Oct 10, 2024 08:57Gazeti la Telegraph la Uingereza limeandika kuwa, Iran imethibitisha uwezo wake wa "kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani" na kwamba kinachofuata baadaye huenda "kinaweza kuwa na uharibu mbaya sana."
-
Iran yataka kutumiwa uwezo wa eneo kukomesha mauaji ya halaiki
Oct 10, 2024 08:53Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ametoa mwito wa kutumika kwa uwezo na suhula zote za eneo la Asia Magharibi ili kusimamisha vita mara moja na kuzuia kuendelea mauaji ya kimbari na uharibifu wa miundo mbinu huko Lebanon na Palestina.
-
Safari ya Waziri Mambo ya Nje wa Iran nchini Saudi Arabia; mlingano wa medani ya mapambano na diplomasia
Oct 10, 2024 01:07Katika uga wa diplomasia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajaribu kwa nguvu zake zote kukabiliana na maovu na uchochezi wa vita vya utawala wa Kizayuni na kuhusiana na suala hilo, Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ameondoka kuelekea Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran afanya mazungumzo na mwenzake wa Saudia
Oct 10, 2024 00:50Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amefanya 'mazungumzo ya kujenga' na mwenzake wa Saudi Arabia Mwanamfalme Faisal bin Farhan mjini Riyadh.
-
Iran yakosoa tuhuma zisizo na msingi za Uingereza
Oct 09, 2024 10:29Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amejibu madai ya afisa wa usalama wa Uingereza akisema: Maafisa wa serikali ya London wanapaswa kutumia ushawishi wao kusimamisha uchokozi na jinai za utawala ghasibu wa Israel badala ya kutoa tuhuma zisizo na msingi na mijadala ya kupotosha.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Wazayuni wanataka kuathiri uchaguzi wa Marekani
Oct 09, 2024 03:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utawala wa Kizayuni unataka kupanua vita katika eneo la Magharibi mwa Asia lengo likiwa ni kuathiri matokeo ya uchaguzi ujao wa Marekani.
-
Rais wa Iran: Ulimwengu wa watoto haupaswi kuchafuliwa na vita na uwaniaji madaraka wa watu wazima
Oct 09, 2024 03:24Rais wa Iran ameeleza kuwa ulimwengu mzuri, wa kuvutia na wa watoto wadogo wasio na hatia haupaswi kuchafuliwa na vita na uwaniaji madaraka wa watu wazima.