The Telegraph: Iran imethibitisha uwezo wake wa kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani
(last modified Thu, 10 Oct 2024 12:27:11 GMT )
Oct 10, 2024 12:27 UTC
  • The Telegraph: Iran imethibitisha uwezo wake wa kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani

Gazeti la Telegraph la Uingereza limeandika kuwa, Iran imethibitisha uwezo wake wa "kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani" na kwamba kinachofuata baadaye huenda "kinaweza kuwa na uharibu mbaya sana."

Telegraph imeandika kuwa, ulimwengu mzima ulitazama kwa unyonge kile kilichotokea usiku wa kuamkia Oktoba 1 kwa utawala wa Israel, na kukaa chini ukiandika maelezo baada ya makombora ya Iran kupenya na kuvuka Iron Dome ya Israel, licha ya ving'ora ambavyo vilikuwa vimepigwa muda mfupi kabla ya tukio hilo.

Itakumbukwa kuwa awali, utawala wa Kizayuni wa Israel ulijaribu kudogesha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Iran, lakini kwa mujibu wa gazeti la "The Telegraph, "wiki moja baada ya shambulio hilo linalotambuliwa kuwa moja ya mashambulizi makali zaidi ya nchi moja katika historia kwa kutumia makombora ya kisasa ya balestiki, athari kamili ya shambulio hilo "zimedhihirika, haswa baada ya utawala huo kukiri kwamba kambi zake kadhaa za kijeshi zimeshabuliwa."

 

Telegraph imesema kuwa Iran imethibitisha uwezo wake wa "kupenya mfumo mkubwa zaidi wa ulinzi wa anga duniani." Kinachofuata kinaweza kuwa maangamizi. Ulimwengu wote ulikuwa ikitazama bila msaada kile kilichotokea usiku wa kuamkia Oktoba 1 kwa Israel, na kuandika tu kumbukumbu za tukio baada ya makombora ya Iran kupenya kwenye mfumo wa Iron Dome wa Israel, licha ya maonyo ambayo yalitolewa muda mfupi kabla ya tukio hilo."

Katika mahojiano na gazeti hilo, wataalamu wameeleza wasiwasi wao kuhusu kasi na ukubwa wa makombora hayo na kujiuliza “je, tezi hii ya saratani, ‘Israel’, itaweza kujilinda dhidi ya mawimbi zaidi ya makombora, iwapo vita vitaendelea kuongezeka katika Mashariki ya Kati?”

Kwa upande wake, Fabian Hoffman, mtaalamu wa makombora na mtafiti katika Mradi wa Nyuklia wa Oslo, ameliambia gazeti hilo kwamba picha zinaonyesha wazi "kasi ya ajabu ya makombora ya Iran."