Mkuu wa Mawaziri Kenya atofautiana na Rais Ruto kuhusu kuwapiga risasi waandamanaji
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128298-mkuu_wa_mawaziri_kenya_atofautiana_na_rais_ruto_kuhusu_kuwapiga_risasi_waandamanaji
Mkuu wa Mawaziri wa Mawaziri nchini Kenya, Musalia Mudavadi ametofautiana na Rais William Ruto kuhusu wito wake wa kupigwa risasi viijana wanaoandamana kupinga sera za serikali yake na amevitaka vyombo vya usalama visiwaumize Wakenya wakati wa maandamano.
(last modified 2025-10-22T06:10:45+00:00 )
Jul 14, 2025 03:13 UTC
  • Musalia Mudavadi
    Musalia Mudavadi

Mkuu wa Mawaziri wa Mawaziri nchini Kenya, Musalia Mudavadi ametofautiana na Rais William Ruto kuhusu wito wake wa kupigwa risasi viijana wanaoandamana kupinga sera za serikali yake na amevitaka vyombo vya usalama visiwaumize Wakenya wakati wa maandamano.

Bw Mudavadi anasema, Wakenya wanatekeleza majukumu yao ya kikatiba. Hata hivyo, amewataka Wakenya wanaoandamana waheshimu haki za wengine kwa kuwa huo ndio msingi wa demokrasia.

“Tufikirie na tutathmini haki zetu ninapowaomba maafisa wetu wa usalama wasiwajeruhi raia wanaoandamana. Wale wanaoandamana nao pia waheshimu haki za wengine,” amesema Bw Mudavadi katika video ambayo imesambaa mitandaoni.

Kauli yake inakuja baada ya matamshi ya Rais William Ruto wiki jana kuwataka polisi wawalenge kwa risasi miguuni watu wanaoandamana ili waende hospitalini na pia kuwajibikia mashtaka kortini.

Rais Ruto alisema japo hajaamrisha wauawe, polisi lazima wakabiliane na wahalifu kwa mujibu wa sheria.