-
EU: Tuko tayari kuboresha ushirikiano na Iran
Jul 07, 2024 04:07Msemaji wa Umoja wa Ulaya anayehusika na sera ya mambo ya nje na usalama amempongeza Rais mteule wa Iran na kusema umoja huo uko tayari kustawisha ushirikiano wa pande mbili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran yashinda viti 2 vya kimataifa katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani
Jul 07, 2024 01:10Bahareh Arabi, Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Hali ya Hewa la Iran amesema wataalamu 2 wa Shirika la Hali ya Hewa la Iran wamechaguliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Huduma ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
-
Kiongozi Muadhamu akutana na Rais mteule wa Iran na Jalili
Jul 06, 2024 23:29Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian na kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Sisitizo la kupanuliwa uhusiano wa Iran na China
Jul 06, 2024 22:54Mohammad Mokhbrr, Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Rais Xi Jinping wa China walikutana na kujadiliana kando ya Mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai huko Astana, mji mkuu wa Kazakhstan.
-
Viongozi wa nchi mbalimbali waendelea kutoa pongezi kwa Rais mteule wa Iran
Jul 06, 2024 22:52Viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa nchi mbalimbali duniani wameendelea kumpongeza Daktari Massoud Pezeshkian kwa kuibuka na ushindi katika duru ya 14 ya uchaguzi wa rais wa Iran.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Suala muhimu zaidi la sasa ni kushindwa nchi za Magharibi kimaadili na kisiasa
Jul 06, 2024 11:35Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa suala muhimu zaidi duniani leo hii ni kufeli nchi za Magharibi katika masuala ya kimaadili na kisiasa.
-
Viongozi wa dunia wamtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Iran
Jul 06, 2024 07:52Marais na viongozi wa nchi mbali mbali duniani wameendelea kutuma jumbe na salamu za pongezi wakimpongeza Rais mteule wa Iran, Massoud Pezeshkian kwa kuibuka na ushindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika ndani na nje ya Iran jana Ijumaa.
-
Jalili ampongeza Pezeshkian kwa ushindi wa kiti cha Rais wa Iran
Jul 06, 2024 11:19Saeed Jalili, ametoa ujumbe akimpongeza Massoud Pezeshkian aliyechuana naye katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu baada ya mapema leo asubuhi Wizara ya Mambo ya Ndani kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana kote nchini.
-
Kiongozi Muadhamu ampongeza Rais mteule wa Iran; awashukuru Wairani kwa kupiga kura kwa wingi
Jul 06, 2024 08:40Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amempongeza Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian na kutoa shukrani za dhati pia kwa wagombea wote wa uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu; na maafisa walioshiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi huo.
-
Masoud Pezeshkian ashinda kiti cha urais Iran
Jul 05, 2024 23:38Massoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa Rais wa 9 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kupata kura nyingi zaidi za wananchi katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika jana Ijumaa.