-
Iran: Kupanuka jinai za Wazayuni ni tishio kwa amani na usalama wa dunia
Jul 29, 2024 09:23Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kupanuka na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ni tishio kwa amani na usalama wa eneo la Maghahribi mwa Asia na dunia.
-
Tehran inajiandaa kwa hafla ya kuapishwa Pezeshkian huku viongozi wa nchi mbalimbali wakiwasili kwa wingi
Jul 29, 2024 09:09Viongozi na maafisa wa ngazi ya juu kutoka nchi mbalimbali tayari wamewasili Tehran mji mkuu wa Iran kwa lengo la kushiriki katika hafla ya kuapishwa Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian kesho Jumanne.
-
Indhari ya Ali Bagheri kwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ujerumani
Jul 28, 2024 23:01Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufungwa vituo vya Kiislamu nchini Ujerumani ni kitendo cha kisiasa kabisa kinachoendana na chuki dhidi ya Uislamu na maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Demokrasia ya Iran haikupatikana kwa urahisi
Jul 28, 2024 08:37Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameutaja uchaguzi wa Rais wa Awamu ya 14 wa Jamhurii ya Kiislamu ya Iran kuwa ni wa mafanikio ya taifa katika mtihani muhimu. Ameyasema hayo leo mjini Tehran katika sherehe ya amemuidhinisha rasmi Rais wa Awamu ya 14 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian.
-
Iran yaionya Israel dhidi ya 'chokochoko mpya' kuhusu Lebanon
Jul 28, 2024 07:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametahadharisha kuhusu chokochoko yoyote mpya ya utawala wa Kizayuni wa Israel mkabala wa Lebanon.
-
Kiongozi Muadhamu amuidhinisha rasmi Dkt Pezeshkian kuwa Rais wa Iran
Jul 28, 2024 04:18Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemuidhinisha rasmi Masoud Pezeshkian kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa wa kitaifa na kijeshi hapa Tehran.
-
Balozi wa Iran Lebanon: Iran daima inaunga mkono amani na utulivu katika eneo
Jul 28, 2024 04:16Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haifuatilii vita na daima imekuwa ikiunga mkono amani na utulivu katika eneo la Asia Magharibi.
-
Zaidi ya wageni 300 kushiriki hafla ya kuapishwa Rais mpya wa Iran
Jul 27, 2024 23:46Zaidi ya wageni 300 watahudhuria hafla ya kuapishwa rais mteule wa Iran Dakta Masoud Pezeshkian.
-
Tehran: Tuhuma za utawala wa Israel unaouawa watoto dhidi ya Iran ni kichekesho
Jul 27, 2024 03:46Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, tuhuma zilizotolewa na waziri wa utawala wa Israel unaoua watoto dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 ni jaribio lililofeli la kupotosha fikra za umma za walimwengu kuhusiana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huu huko Gaza.
-
Iran yapongeza makubaliano ya makundi ya Palestina ya Beijing China
Jul 26, 2024 23:06Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amekitaja kikao cha hivi karibuni cha makundi ya Palestina mjini Beijing China na makubaliano yaliyofikiwa kuwa ni katika mwelekeo wa mapatano na maridhiano ya kitaifa. Nasser Kan'ani Chafi amesema hiyo ni hatua yenye thamani kubwa na "harakati ya kuelekea katika mwelekeo sahihi".