-
Msisitizo wa Iran juu ya haki yake katika medani ya gesi ya Arash
Mar 28, 2024 02:20Naibu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Sheria, Mohammed Dehghan, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitafumbia jicho kwa hali yoyote ile haki zake katika medani ya pamoja ya gesi ya Arash na haitaruhusu upande wowote kukiuka sheria za kimataifa katika suala hili.
-
Rais wa Iran: Palestina sasa ni kadhia ya ulimwengu wa ubinadamu
Mar 27, 2024 23:41Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kutokana na muqawama au mapambano ya Kiislamu na misimamo imara ya wananchi wanaodhulumiwa na wenye nguvu wa Gaza, kadhia ya Palestina sasa imevuka mipaka ya ulimwengu wa Kiislamu na kuwa suala la ulimwengu wa ubinadamu.
-
Wairani wawaenzi mashahidi wa Kipalestina katika hafla ya makumi ya maelfu
Mar 27, 2024 22:48Zaidi ya Wairani 100,000 wamehudhuria sherehe kubwa ya kidini katika uwanja wa michezo wa Azadi ambapo kati ya mambo mengine wamewaenzi mashahidi Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Iran yazitaka IPU, NAM kufanya juhudi za kusitisha vita Gaza
Mar 27, 2024 04:11Iran imetoa mwito kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Mabunge (IPU) na Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) kuchukua hatua za maana na za kivitendo kusitisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Haniya: Azimio la Baraza la Usalama linaonesha Israel imetengwa duniani
Mar 27, 2024 04:10Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umetengwa vibaya na dunia kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa; siku moja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio la kutaka kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza.
-
Safari ya pili ya Haniyeh mjini Tehran baada ya operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa
Mar 27, 2024 02:57Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, aliwasili Jumanne ya jana mjini Tehran ikiwa ni safari yake ya pili baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
-
Kiongozi Muadhamu: Muqawama usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu
Mar 26, 2024 23:28Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, Muqawama usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu.
-
"Siku ya Quds imebakisha hai kadhia ya Palestina"
Mar 26, 2024 22:38Mkuu wa Makao Makuu ya Intifadha na Siku ya Quds ya Iran amesema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yana umuhimu mkubwa katika kubakisha hai kadhia ya ukombozi wa Palestina.
-
Ismail Haniya wa Hamas afika Tehran, akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
Mar 26, 2024 08:12Ismail Haniyah, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), leo amewasili Tehran na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian ambapo wamejadili matukio ya hivi karibuni katika eneo la Ukanda wa Gaza.
-
Nasser Kanani: Hatua ya Baraza la Usalama la UN kuhusu kusimamisha vita Gaza haitoshi
Mar 26, 2024 04:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hatua ya Baraza la Usalama kuhusu kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza haitoshi. Amesema, hatua muhimu, zaidi ya kupasisha azimio hilo ni kuchukuliwa hatua athirifu ili kufanikisha utekelezaji wa azimio hilo na kusitisha kikamilifu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuondoa kikamilifu mzingiro wa kidhulma dhidi ya Gaza.