-
Abdollahian: Tunafuata taratibu za kisheria na kimataifa kuhusu shambulio la kigaidi la Kerman
Jan 04, 2024 08:58Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo kuwa, wizara yake kwa kuzingatia data za awali zilizopatikana kutoka vyanzo rasmi, imeanza kuchukua hatua za haraka za kisheria na kimataifa kupitia Umoja wa Mataifa kuhusu tukio la kigaidi lililotokea jana katika mji wa Kerman.
-
Ugaidi, njama iliyoshindwa ya maadui dhidi ya Iran ya Kiislamu
Jan 04, 2024 08:31Maadui wa Iran ya Kiislamu kwa mara nyingine tena wamewaua shahidi na kuwajeruhi mamia ya raia katika kitendo cha kigaidi.
-
Raisi: Mauaji ya kigaidi hayatatizi umoja, usalama na stratejia ya taifa la Iran
Jan 04, 2024 03:15Rais Sayyid Ebrahim Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kwa simu na mwenzake wa Uturuki na kueleza kuwa: Maadui wa taifa la Iran wanadhani kuwa kwa kustafidi na wenzo wa mauaji ya kigaidi wanaweza kufikia malengo yao haramu lakini taifa la Iran limethibitisha kuwa jinai za aina hiyo haziwezi kuvuruga umoja, usalama na stratejia ya taifa hili.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani: Iran itatoa jibu kali na la haraka kwa mashambulizi ya kigaidi ya Kerman
Jan 04, 2024 03:04Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema kuwa vikosi vya usalama na ulinzi vya nchi hii vitatoa jibu la haraka na kali kwa wahusika wa mashambulizi ya kigaidi yaliyoua watu zaidi ya 100 katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.
-
Kiongozi: Watenda jinai watambue kuwa, wanamapambano wa njia ya Solaimani hawahimili jinai zao
Jan 04, 2024 00:02Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kufuatia kuuawa shahidi makumi ya wafanya ziara wa Shahid Qassem Soleimani na kusisitiza kuwa, wanaotenda jinai watambue kuwa wanamapambano wa njia ya Soleimani hawawezi kuhimili na kuvumilia jinai zao.
-
Dunia yaendelea kulaani miripuko ya kigaidi ya Kerman, Iran, iliyoua watu 95
Jan 03, 2024 23:40Shambulio la kigaidi la lililoua makumi ya watu katika mji wa Kerman wa kusini mashariki mwa Iran linaendelea kulaaniwa katika kona mbalimbali za dunia. Watu 95 wamethibirishwa kuuawa shahidi na 284 wengine wamejeruhiwa.
-
Watu 103 wauawa katika shambulio la kigaidi la Kerman Iran
Jan 03, 2024 09:45Kwa akali watu 103 wameuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia milipuko kadhaa iliyotokea katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.
-
Kuongezeka uwepo wa wanamaji wa Iran katika Bahari Nyekundu
Jan 03, 2024 08:31Meli ya kivita ya Alborz imerudi tena katika Bahari Nyekundu ikiwa ni katika Meli za Kikosi cha 94 cha Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kupitia Lango-Bahari la Bab al-Mandab. Manowari hiyo ya Alborz ilijiunga na Meli za Kusini za Jeshi la Wanamaji Desemba 2019 baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na kuwekwa humo mifumo mipya ya kiteknolojia.
-
Kiongozi Muadhamu: Mkakati mkuu wa Iran ni kutegemea nguvu laini
Jan 03, 2024 08:16Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mkakati mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hiki cha miaka 45 iliyopita ni kutegemea nguvu laini na nguvu hizo zinapaswa zifanywe kubwa zaidi.
-
Amir-Abdollahian: Jinai za utawala wa Kizayuni zimepiga kengele ya hatari katika ukanda huu mzima
Jan 03, 2024 07:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jinai na mauaji ya kigaidi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni nje ya mipaka ya Palestina ni tishio kwa usalama na ni kengele ya hatari kwa amani ya ukanda huu mzima.