Dunia yaendelea kulaani miripuko ya kigaidi ya Kerman, Iran, iliyoua watu 95
Shambulio la kigaidi la lililoua makumi ya watu katika mji wa Kerman wa kusini mashariki mwa Iran linaendelea kulaaniwa katika kona mbalimbali za dunia. Watu 95 wamethibirishwa kuuawa shahidi na 284 wengine wamejeruhiwa.
Umoja wa Mataifa, serikali za Ufaransa, Ireland, Bahrain, Holland, Chuo Kikuu cha al Azhar cha Misri, Umoja wa Ulaya, Norway, Qatar, Saudi Arabia, Uturuki n.k, ni miongoni mwa waliolaani miripuko hiyo miwili ya kigaidi na wametoa mkono wa pole kwa taifa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Tasnim ambalo limeongeza kuwa, nchi nyingine zimejiunga na dunia kulaani jinai hizo za magenge ya kigaidi yanayoungwa mkono na utawala wa Kizayuni wa Israel na madola ya kibeberu hasa Marekani.
António Manuel de Oliveira Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa na kulaani jinai hiyo ya kigaidi na pia ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa miripuko hiyo.
Amma katika woga wake wa kulipiziwa kisasi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, utawala wa Kizayuni wa Israel umewaambia waungaji mkono wake kuwa eti haukuhisika kivyovyote vile na jinai hiyo ya mjini Kerman, Iran.
Gazeti la Marekani la Wall Street Jouranl limeunukuu utawala wa Kizayuni ukidai katika taarifa yake kwa waitifaki wake kwamba eti haukuhusika kwa hahli yoyote ile miripuko hiyo.
Miripuko miwili ya kigaidi ilitokea jana Jumatano huko Kerman, kusini mashariki mwa Iran wakati watu walipokuwa kwenye kumbukumbu za mwaka wa nne wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH. Miripuko hiyo imetokea karibu na kaburi la shahidi huyo mujahid.