Watu 103 wauawa katika shambulio la kigaidi la Kerman Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i106772-watu_103_wauawa_katika_shambulio_la_kigaidi_la_kerman_iran
Kwa akali watu 103 wameuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia milipuko kadhaa iliyotokea katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 03, 2024 09:45 UTC
  • Watu 103 wauawa katika shambulio la kigaidi la Kerman Iran

Kwa akali watu 103 wameuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia milipuko kadhaa iliyotokea katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.

Ripoti za awali zinasema kuwa, milipuko miwili mikubwa imetokea leo katika mji wa Kerman kwenye njia inayoelekea katika makaburi ya mashahidi mjini Kerman.

Milipuko hiyo imetokea wakati watu walipokuwa wakielekea katika makaburi hayo ya mashahidi kwa ajili ya hauli na kumbukumbu ya mwaka wa nne wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, milipuko hiyo pacha imetokea jirani makaburi ya mashahidi mjini Kerman  ambapo ndipo lilipo kaburi la shahidi Qassem Soleimani.

 

Hadi tunaandika habari hii magari ya wagonjwa yalikuwa katika juhudi za kuhamishwa majeruhi kwa ajili ya kuwapeleka hospitali.

Baadhi ya duru za habari ikiwemo Kanali ya Televisheni ya al-Alam zimenukuuu Naibu Mkuu wa Mkoa wa Kerman akitangaza kwamba, tukio hilo ni hujuma ya kigaidi iliyowalenga watu wasio na hatia yoyote. Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi.