-
Kuuawa shahidi, zawadi ya juhudi kubwa alizofanya Sayyid Razi katika umri wake
Dec 29, 2023 05:07Mazishi ya mwili wa Sayyid Razi Mousavi yalifanyika jana Alhamisi mjini Tehran ambapo umati mkubwa wa wananchi na viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walihudhuria.
-
Iran: Tuna uwezo wa kupiga nukta yoyote ya Israel wakati wowote tunapopenda
Dec 29, 2023 01:52Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Iran ina uwezo mkubwa wa kiulinzi kiasi kwamba leo hii inaweza kupiga nukta yoyote ya Israel kwa makombora yanayopiga vizuri mno shabaha, wakati wowote itakapoona kuna haja ya kufanya hivyo.
-
Amir-Abdollahian: Marekani ni kidhabi inapodai haitaki vita vienee; mahandaki ya HAMAS yanafika nje ya Ghaza
Dec 28, 2023 23:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Marekani inaendelea kuusheheneza silaha nzito utawala wa Kizayuni wa Israel bila ya kusita na halafu inadai kuwa eti haitaki vita vya Ghaza vienee nje ya mipaka ya ukanda huo.
-
Hamas yaitaarifu Iran: Tunaweza kukabiliana na Israel Ukanda wa Gaza kwa miezi kadhaa
Dec 28, 2023 22:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, amesema Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeifahamisha Jamhuri ya Kiislamu kwamba ina uwezo wa kutosha kuendeleza mapambano na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa kwa miaka kadhaa.
-
SEPAH: Kisasi cha mauaji ya Jenerali Razi Mousavi kitakuwa maangamizi kwa Israel
Dec 28, 2023 08:44Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) anasema kuwa, kisasi cha Iran kwa jinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumuua kigaidi mshauri mkuu wa kijeshi nchini Syria hakitakuwa chochote bali ni kuutokomeza kabisa utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu mtazamo wa kimantiki na wa hoja wa Uislamu kuhusu wanawake
Dec 28, 2023 08:12Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutana na maelfu ya wanawake na wasichana na kubainisha mtazamo wa kimantiki na kiakhlaqi wa Uislamu kuhusu nyuga mbalimbali za uwepo wa wanawake katika familia na shughuli zao zisizo na kikomo katika jamii, katika uga wa siasa na katika kusimamia majukumu katika ngazi mbalimbali.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi asalisha Sala ya Maiti ya kuusalia mwili wa Shahidi Mousavi
Dec 28, 2023 03:16Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi ameongoza Sala ya Maiti ya kuusalia mwili wa Kamanda Shahidi Sayyid Razi Mousavi pamoja na kumsomea Faatiha na kumuombea dua Shahidi huyo.
-
Mwandishi habari: Palestina itakuwa huru iwapo Waislamu wote wataisaidia kama inavyofanya Iran
Dec 28, 2023 01:55Mwandishi wa habari kutoka Ukanda wa Gaza amepongeza uungaji mkono usioyumba wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina kwa miongo kadhaa sasa na kuongeza kwamba, ardhi za Palestina zingekombolewa kutoka mikononi mwa ukoloni na uvamizi wa Israel ikiwa serikali zote za Kiislamu zingesaidia Wapalestina kama Iran inavyofanya.
-
Mazungumzo ya Amir-Abdollahian na viongozi wa Armenia
Dec 28, 2023 00:53Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran aliyeko safarini nchini Armenia amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo.
-
Lavrov: Russia inaheshimu bila masharti mamlaka ya ardhi yote ya Iran
Dec 28, 2023 00:52Sergei Lavrov Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa, Russia inaheshimu kwa dhati na kiukwelii kabisa tena bila masharti mamlaka ya ardhi yote ya ardhi ya Iran na kwamba, huu ni msimamo usiobadilika wa Moscow.