Dec 28, 2023 04:23 UTC
  • Mazungumzo ya Amir-Abdollahian na viongozi wa Armenia

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran aliyeko safarini nchini Armenia amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo.

Katika mazungumzo yake hayo, Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran amejadili na kubadilishana mawazo na viongozi hao kusiana na uhusiano wa pande mbili na matukio ya kieneo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akiuongoza ujumbe wa nchi yake jana aliwasili Yerevan kwa mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa Armenia ambapo amekutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan. Inaonekana kwamba matukio ya hivi karibuni katika Caucasia Kusini na mahusiano ya nchi mbili ndio ajenda kuu ya mazungumzo haya.

Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa nchini Armenia

 

Safari ya Hossein Amir-Abdollahian nchini Armenia inafanyika katika hali ambayo, hivi karibuni Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Nikol Pashinyan, Waziri Mkuu wa Armenia.

Katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa, kustawisha uhusiano wa ujirani na kuimarishwa mahusiano ili kuhakikisha manufaa ya pande zote mbili na maslahi ya nchi za eneo hili ni siasa za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tags