-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mtazamo wa Magharibi kuhusu mwanamke ni wa kimaslahi
Dec 27, 2023 10:57Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kislamu mapema leo amehutubia maelfu ya wanawake na wasichana ambako amebainisha mtazamo wa kimantriki wa Uislamu kuhusu nafasi ya wanawake katika familia na shughuli kijamii, siasa na uongozi katika ngazi mbalimbali na kusisitiza kuwa: Katika Uislamu, njia ya shughuli zozote za kijamii ziko wazi kwa wanawake, sawa na ilivyo kwa wanaume, kwa sharti kwamba mambo mawili muhimu yazingatiwe, yaani suala la familia na kuchunga hatari ya mvuto wa kijinsia.
-
IRGC: Israel isubiri kisasi chetu kwa mauaji ya kamanda Sayyid Razi Mousavi
Dec 27, 2023 10:56Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Iran itatoa jibu ipasavyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya mauaji ya mshauri mkuu wa kijeshi wa IRGC nchini Syria, na ameahidi kulipiza kisasi kwa shambulio hilo la kigaidi katika nyakati na maeneo tofauti.
-
Jenerali Baqeri: Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua kamanda wa IRGC
Dec 27, 2023 03:18Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Iran amesema Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua shahidi Kamanda Sayyid Razi Mousavi, aliyekuwa mshauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni haitapita hivi hivi bila kujibiwa.
-
Sisitizo la Amir-Abdollahian la kutatuliwa matatizo kati ya Iran na Afghanistan
Dec 26, 2023 23:22Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kutatuliwa masuala yaliyopo kati ya Iran na Afghanistan yakiwemo masuala ya mipaka na maji.
-
Maafisa wa jeshi la Syria washiriki katika hitma ya shahidi Brigedia Jenerali Razi Mousavi
Dec 26, 2023 08:29Maafisa wa kijeshi na wa jeshi la Syria leo Jumanne wameshiriki katika hitma ya shahidi Brigedia Jenerali Sayyid Razi Mousavi katika ubalozi wa Iran huko Damascus, Syria.
-
Radiamali mbalimbali za kuuawa shahidi mshauri wa kijeshi wa Iran nchini Syria
Dec 26, 2023 05:28Kamanda Sayyid Razi Mousavi, mmoja wa washauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH), ambaye alikuwa akifanya kazi katika uga wa utoaji misaada ya kilojistiki kwa Mhimili wa Muqawama wa Syria, aliuawa shahidi katika shambulio lililofanywa jana Jumatatu na utawala wa Kizayuni katika eneo la Zainabiyah mjini Damascus.
-
Raisi: Israel italipa gharama ya kumuua mshauri wa kijeshi wa IRGC
Dec 25, 2023 23:53Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utalipa gharama ya kitendo chake cha uhalifu cha kumuua mshauri mkuu wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Syria.
-
Iran: Marekani haina ustahiki kuwatuhumu wengine; inachukiwa zaidi kwa kuiunga mkono Israel
Dec 25, 2023 23:29Iran imepuuzilia mbali shutuma "zisizo na thamani" za Marekani kwamba inazidisha mvutano katika bahari kuu, ikisema Washington, ambayo ni mshirika katika vita vya mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel kwenye Ukanda wa Gaza, "haina ustahiki" wa kutoa madai dhidi ya Tehran.
-
Radiamali ya Amir Abdollahian kwa madai ya Marekani kuhusu hatua ya Yemen dhidi ya meli za Israel
Dec 25, 2023 23:09Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kuwa Iran haina askari wa niaba katika eneo la Asia Magharibi amesisitiza kuwa, Iran haihusiki na mashambulizi ya Yemen dhidi ya meli za Israel.
-
"Ubeberu wa US unaporomoka, muqawama ndiyo nguzo ya usalama katika eneo"
Dec 25, 2023 07:13Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Wamarekani wamekiri wenyewe kwamba, nidhamu ya dunia iliyojengeka katika misingi ya ubeberu ipo katika mkondo wa kuporomoka, na kwamba mabeberu hawawezi kuendelea kuwatwisha walimwengu misimamo na mitazamo yao.