Jenerali Baqeri: Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua kamanda wa IRGC
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i106474-jenerali_baqeri_israel_imefanya_kosa_la_kistratejia_kwa_kumuua_kamanda_wa_irgc
Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Iran amesema Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua shahidi Kamanda Sayyid Razi Mousavi, aliyekuwa mshauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni haitapita hivi hivi bila kujibiwa.
(last modified 2023-12-27T03:18:59+00:00 )
Dec 27, 2023 03:18 UTC
  • Jenerali Baqeri: Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua kamanda wa IRGC

Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Iran amesema Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua shahidi Kamanda Sayyid Razi Mousavi, aliyekuwa mshauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni haitapita hivi hivi bila kujibiwa.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri aliyasema hayo jana Jumanne katika taarifa na kueleza kuwa, shambulio la anga la kioga la Israel lililoua Jenerali Mousavi mjini Damascus lilikiuka wazi mamlaka ya kujitawala Syria.

Ameongeza kuwa, hujuma hiyo ya kijinai ya Israel mbali na kukanyaga hati na sheria za kimataifa, lakini vie vile imefichua dhati ya ugaidi ya utawala wa Kizayuni.

Meja Jenerali Baqeri ameeleza bayana kuwa, hatua yoyote ya kigaidi na kiwendawazimu ya Israel haitausaidia utawala huo pandikizi, na badala yake itaendelea kuchochea moto wa muqawama dhidi yake.

Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, Israel haijaambulia chochote katika mashambulio na jinai zake huko Gaza, na kwamba kuendelea kwa ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kumefichua sura halisi za Wazayuni wanaoua watoto na washirika wao wahalifu.

Makundi ya muqawama pia yamelaani mauaji ya Kamanda Razi

Meja Jenerali Mohammad Baqeri amesisiitiza kuwa: Israel imefanya kosa la kistratejia kwa kumuua shahidi Kamanda Sayyid Razi Mousavi, aliyekuwa mshauri wa Kikosi cha Quds cha SEPAH nchini Syria.

Kamanda Sayyid Razi Mousavi aliuawa shahidi katika shambulizi la anga la Israel katika kitongoji cha Sayyida Zainab katika mji mkuu wa Syria, Damascus mapema juzi Jumatatu.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi, alisema utawala wa Kizayuni wa Israel utalipa gharama ya kitendo chake cha uhalifu cha kumuua mshauri huyo mkuu wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Syria.