-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni mwanzo wa kufutika athari za Marekani
Dec 01, 2023 08:25Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuhusiana na matukio ya Gaza kwamba: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni mwanzo wa kufutika athari za Marekani.
-
Iran: Wanyonyaji damu wa Kizayuni wameanzisha upya mauaji Gaza kwa uungaji mkono wa US
Dec 01, 2023 07:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: baada ya kuwaua zaidi ya Wapalestina 15,000, wanyonyaji damu wa Kizayuni wameanzisha duru mpya ya mauaji huko Gaza kwa uungaji mkono kamili wanaoendelea kupewa na serikali ya Marekani.
-
IRGC: Israel itatoweka ndani ya saa 24 kwa Kimbunga kingine cha al-Aqsa
Dec 01, 2023 03:47Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilibainisha wazi kuwa kuporomoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuko karibu zaidi na ni sahali zaidi ya ilivyodhaniwa.
-
Rais wa Iran asusia mkutano wa COP28 Dubai kwa kushiriki Israel
Dec 01, 2023 03:17Rais Ebrahim Raisi wa Iran hatashiriki mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, mjini Dubai kutokana na uwepo wa Rais Isaac Herzog na maafisa wengine wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye mkutano huo.
-
Iran yaipongeza Yemen kwa kuwaunga mkono Wapalestina
Nov 30, 2023 23:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepongeza na kusifu uungaji mkono wa Yemen kwa taifa la Palestina, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni umeshadidisha jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Amir Abdollahian apongeza msimamo wa Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni
Nov 30, 2023 02:05Katika barua yake kwa Musa Faki, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshukuru msimamo wa afisa huyo wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika wa kulaani kushambuliwa kwa mabomu hospitali ya Al-Maamadani na utawala wa Kizayuni na kutoa wito wa kusitishwa mashambulizi mengine kama hayo na kutaka kutolewa misaada ya kibinadamu ya haraka kwa wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
-
Iran: Afrika ina hamu ya kufufua utambulisho wake
Nov 30, 2023 00:23Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa amesisitizia haja ya kuimarishwa uhusiano na ushirikiano wa Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika ikiwemo Senegal katika nyuga mbalimbali.
-
Iran: Hatima ileile ya kutoroka Afghanistan itawafika askari wa Marekani waliopiga kambi Iraq na Syria
Nov 30, 2023 03:47Mshauri wa ngazi ya juu wa kijeshi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amepongeza Kambi ya Muqawama katika eneo na kusema "kutoroka" ndio hatima ya mwisho itakayovifika vikosi vamizi vya jeshi la Marekani nchini Syria na Iraq kama ilivyotokea Afghanistan.
-
Kiongozi Muadhamu: Kimbunga cha al Aqsa cha Hamas dhidi ya Israeli, kimepindua meza ya ajenda ya kisiasa ya Marekani
Nov 29, 2023 08:29Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei anasema tukio la kihistoria la Kimbunga cha al-Aqsa cha harakati ya Hamas kimsingi lilikuwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini limeweza kuvuruga sera za Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia na litaifuta kabisa ajenda hiyo.
-
Kiongozi wa Mapinduzi asisitiza juu ya kuimarishwa utayari wa kivita wa jeshi la wanamaji.
Nov 29, 2023 08:14Akizungumza karibuni katika kikao na Kamanda Mkuu pamoja na makamanda wengine wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uwezo mkubwa wa jeshi hilo hasa katika utekelezaji wa siasa za kiuchumi baharini na kusisitiza ulazima wa kuvumbuliwa uwezo mpya kwa ajili ya kuimarisha Mfumo na taifa na vilevile kuleta matumaini na uchangamfu katika jamii.