-
Tume ya Haki za Binadamu ya Iran: Utawala wa Kizayuni hautakwepa kesi mahakama ya ICC
Nov 25, 2023 01:04Katibu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu inalipa mazingatio maalumu suala la kuhakikisha utawala wa Kizayuni wa Israel haukwepi kesi ya kutenda uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
-
Shekhe Kazem Seddiqi: Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa ilivunja uti wa mgongo wa Israel
Nov 24, 2023 09:12Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imevunja mgongo wa Israel kwa kutegemea imani na ushujaa katika operesheni ya Kimbunga ya Al-Aqswa.
-
Amir-Abdollahian: Uungaji mkono wa Marekani kwa Israel ulisababisha kuendelea kwa vita Gaza
Nov 24, 2023 08:32Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kama si msaada na himaya ya Marekani kwa utawala ghasibu wa Israel, utawala huo bandia haungeweza kuendeleza vita na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
-
Kan'ani: Usitishaji vita Gaza ni hatua ya kwanza ya kusitisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni
Nov 24, 2023 02:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa usitishaji vita wa muda wa kibinadamu uliofikiwa Ukanda wa Gaza ni hatua ya awali kuelekea kusitisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni unaouwa watoto.
-
Kiongozi Muadhamu; kushindwa Wazayuni hakutafidiwa kwa jinai
Nov 23, 2023 23:20Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika kikao na washindi wa nishani za Michezo ya Asia na Para-Asia huko Hangzhou na wanamichezo wengine wa Iran kuwa, mienendo yao ya heshima katika medani za michezo ni dhihirisho la sura ya taifa la Iran, na kusema kuhusu matukio ya Gaza kuwa utawala wa Kizayuni, pamoja na jinai zake zote, haujaweza na wala hautaweza kufidia kushindwa kwake kukubwa kwake hivi karibuni na katika mustakbali.
-
Raisi: Israel haijaambulia chochote katika vita vyake Gaza
Nov 23, 2023 04:05Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Israel imefeli kufikia malengo yake yote katika hujuma na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Eslami: IAEA iache kuingiza siasa kwenye kesi ya Iran
Nov 22, 2023 23:37Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) ameutaka Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ujiepushe na tabia ya kuingiza siasa kwenye faili la nyuklia la Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Israel ilipata pigo katika Operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa
Nov 22, 2023 09:01Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema utawala haramu wa Israel "iliangushwa" katika Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, operesheni kubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kufanywa na makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina dhidi ya utawala huo ghasibu.
-
Rais wa Iran: Matukio Gaza ni nembo ya kuporomoka kimaadili Wamagharibi
Nov 22, 2023 03:10Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Gaza ni ishara na mfano wa wazi wa kuporomoka kwa maadili ya nchi za Magharibi na kuongeza kuwa, uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na Magharibi kwa mauaji ya halaiki na mauaji ya watoto wachanga huko Gaza ni jambo baya zaidi kuwahi kutokea kwa ubinadamu.
-
Meja Jenerali Baqeri: Kuua watoto si ushindi kwa Waisraeli waliofeli; Ushindi wa Wapalestina unakaribia
Nov 22, 2023 00:01Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Iran amesema kuwa mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza hayana maana ya ushindi kwa utawala huo ghasibu, akibainisha kwamba ushindi wa mwisho wa taifa la Palestina uko kwenye upeo wa macho.