-
Meja Jenerali Salami: Matunda yote ya Magharibi yamesombwa na Kimbunga cha Al-Aqsa
Nov 21, 2023 09:43Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema matunda yote ya Marekani, nchi za Magharibi, na Wazayuni yameyoyoma na kusombwa na operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
-
Amir Abdollahian: Tunaendelea kutoa msaada wa kisiasa kwa muqawama
Nov 21, 2023 04:33Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa na hapa ninamnukuu: "Hatukuwepo katika oparesheni ya Hamas, na huo ulikuwa uamuzi wa Palestina kikamilifu," mwisho wa kunukuu. Abdollahian amesisitiza kuwa: 'Tutaendelea kuunga mkono kisiasa muqawama mkabala wa Maghasibu Wazayuni.'
-
Mkuu wa IRGC: Israel imeshindwa, Wapalestina ndio washindi
Nov 21, 2023 02:04Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umeshindwa na wapigania ukombozi (wanamuqawama) wa taifa la Palestina na kuwa utawala huo umeshindwa kutokana na makosa yake wenyewe.
-
BRICS, kwa ombi la Iran, kufanya mkutano wa dharura kujadili Gaza
Nov 20, 2023 23:46Kufuatia pendekezo la Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kundi la BRICS linatazamiwa kufanya mkutano wa dharura kujadili vita vya uvamizi vya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Rais wa Iran awaandikia barua wakuu wa nchi 50 kuhusu jinai za Israel huko Ghaza
Nov 20, 2023 11:24Rais Ebrahim Raisi amewaandikia barua wakuu na viongozi wa nchi 50 duniani kuwahimiza kuwa na kauli moja kuhusu wajibu wa kukomeshwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Ghaza.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza udharura wa kudumishwa kasi ya maendeleo ya kijeshi
Nov 20, 2023 04:24Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja mafanikio ya kisayansi hapa nchini kuwa ni matokeo ya nia inayotegemea azma na imani thabiti na kusisitiza kuwa: Popote pale ambapo vijana wetu waliingia kwa azma na imani wameweza kufanya mambo makubwa; na maonyesho haya ni kielelezo cha dhamira na imani hiyo.
-
Raisi: Damu za mashahidi wa Palestina zitaleta nidhamu ya dunia yenye uadilifu
Nov 19, 2023 11:06Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema 'nidhamu mpya ya dunia yenye uadilifu' itaibuka kutokana na damu za wananchi wa Palestina zilizomwagwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Iran yazindua kombora la hypersonic la 'Fattah 2'
Nov 19, 2023 09:51Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua kombora jipya la hypersonic lililopewa jina la 'Fattah 2'.
-
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi: Kadhia za Gaza zimewadhihirishia walimwengu hakika nyingi zilizofichika
Nov 19, 2023 09:41Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: kadhia za Gaza zimewadhihirishia walimwengu hakika nyingi zilizofichika, na moja wapo ya hakika hizo ni uungaji mkono wa viongozi wa nchi za Magharibi kwa ubaguzi wa rangi.
-
Kan'ani Chafi: Mashambulio dhidi ya hospitali yamefichua zaidi hulka ya kijinai ya utawala wa Kizayuni
Nov 18, 2023 23:42Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, mashambulio dhidi ya hospitali yanakinzana na vigezo vyote vya haki za binadamu, sheria za kimataifa na hati ya makubaliano ya Geneva na kubainisha kwamba, mashambulio ya utawala haramu wa Israel dhidi ya hospitali yamedhihirisha zaidi hulka na dhati ya kijinai ya utawala huo ghasibu.