Amir Abdollahian: Tunaendelea kutoa msaada wa kisiasa kwa muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i105056-amir_abdollahian_tunaendelea_kutoa_msaada_wa_kisiasa_kwa_muqawama
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa na hapa ninamnukuu: "Hatukuwepo katika oparesheni ya Hamas, na huo ulikuwa uamuzi wa Palestina kikamilifu," mwisho wa kunukuu. Abdollahian amesisitiza kuwa: 'Tutaendelea kuunga mkono kisiasa muqawama mkabala wa Maghasibu Wazayuni.'
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 21, 2023 04:33 UTC
  • Amir Abdollahian: Tunaendelea kutoa msaada wa kisiasa kwa muqawama

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa na hapa ninamnukuu: "Hatukuwepo katika oparesheni ya Hamas, na huo ulikuwa uamuzi wa Palestina kikamilifu," mwisho wa kunukuu. Abdollahian amesisitiza kuwa: 'Tutaendelea kuunga mkono kisiasa muqawama mkabala wa Maghasibu Wazayuni.'

Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mahojiano na televisheni ya CBS News mjini Geneva Uswisi kuhusu matukio ya Gaza kwamba: Utawala wa Israel unapatiwa silaha za vita ikiwemo zile zilizopigwa marufuku kutoka katika kambi zote za kijeshi katika eneo; jambo linalomaanisha kuwa Marekani inahusika waziwazi katika vita dhidi ya Gaza na mauaji ya halaiki katika eneo hilo.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: Wahouthi ni sehemu muhimu ya jamii na mfumo wa sasa wa kisiasa wa Yemen, na wanafanya maamuzi na kutenda ndani ya mfumo kwa maslahi yao, ingawa walitangaza wazi kwamba hawatakuwa na msimamo tofauti kuhusu mauaji ya kimbari yanayojiri huko Gaza. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amebanisha kuwa: Makundi yaliyopo Iraq na Syria yanachukua hatua dhidi ya maslahi ya Marekani; yamechukua hatua kulingana na maamuzi yao."