Nov 20, 2023 14:54 UTC
  • Rais wa Iran awaandikia barua wakuu wa nchi 50 kuhusu jinai za Israel huko Ghaza

Rais Ebrahim Raisi amewaandikia barua wakuu na viongozi wa nchi 50 duniani kuwahimiza kuwa na kauli moja kuhusu wajibu wa kukomeshwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Ghaza.

Katika barua yake hiyo muhimu sana kwa wakuu wa nch 50 zikiwemo za Russia, China, Uturuki, Kenya, Afrika Kusini, Kazakhstan na Jordan, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria jinai za kutisha na za kinyama zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ghaza na ambazo zimeshasababisha kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina 12,000 na kuharibiwa kikamilifu miundombinu ya ukanda huo uliozingirwa kwa miaka mingi na kusisitiza kuwa, kinachotarajiwa kutoka kwa nchi huru duniani, ni kusimama pamoja na wananchi wa Palestina. 

Amesema, kwa zaidi ya siku 45 sasa, wanajeshi makatili wa Israel wanafanya jinai za kutisha dhidi ya watoto wachanga, watoto wadogo, wanawake, vizee na watu wa kawaida huko Ghaza na kwamba ni wajibu wa nchi huru hasa za Kiislamu kulisaidia kwa kila namna taifa madhlumu la Palestina ikiwa ni pamoja na kwa njia za kidiplomasia na kiuchumi na kuushinikiza utawala wa Kizayuni ukomeshe jinai zake dhidi ya watu wasio na hatia.

Historia ya Indonesia ya mjini Ghaza baada ya kushambuliwa kikatili na Israel

 

Rais wa Iran amezilaumu baadhi ya nchi za Magharibi kwa misimamo yao ya kindumilakuwili na kudharau kwao kwa makusudi misingi ya kibinadamu, kimaadili na kisheria na kuzitaka nchi huru kushirikiana na kuwa na msimamo na kauli moja ili kukomesha ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Mashambulio ya wanajeshi madhalimu wa Israel dhidi ya Ghaza na kuendelea kwao kuua kinyama watoto wadogo, wanawake na raia wa kawaida wa Kipalestina kunaendelea katika hali ambayo nchi za Magharibi kama Marekani zinaendelea kuikingia kifua kikamilifu Israel na kuzuia hatua zozote za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa za kukomesha jinai hizo.

Tags