Rais wa Iran: Matukio Gaza ni nembo ya kuporomoka kimaadili Wamagharibi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i105094-rais_wa_iran_matukio_gaza_ni_nembo_ya_kuporomoka_kimaadili_wamagharibi
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Gaza ni ishara na mfano wa wazi wa kuporomoka kwa maadili ya nchi za Magharibi na kuongeza kuwa, uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na Magharibi kwa mauaji ya halaiki na mauaji ya watoto wachanga huko Gaza ni jambo baya zaidi kuwahi kutokea kwa ubinadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 22, 2023 03:10 UTC
  • Rais wa Iran: Matukio Gaza ni nembo ya kuporomoka kimaadili Wamagharibi

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Gaza ni ishara na mfano wa wazi wa kuporomoka kwa maadili ya nchi za Magharibi na kuongeza kuwa, uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na Magharibi kwa mauaji ya halaiki na mauaji ya watoto wachanga huko Gaza ni jambo baya zaidi kuwahi kutokea kwa ubinadamu.

Rais wa Iran amesema hayo katika mkutano maalumu wa Jumuiya ya Brics uliofanyika kwa njia ya mawasiliano ya intaneti na ulioutishwa kwa ajili ya kujadilii vita vya Gaza ambapo amekosoa vikali katika hotuba yake uungaji mkono wa Marekani na washirika wake kwa utawala haramu wa Israel.

Aidha akihutubia katikak mkutano huo wa dharura wa BRICS, Rais Ebrahim Raisii amesema, Marekani imeyatafanya mashirika yote ya kimataifa kutokuwa na maana wala utambulisho.

Mkutano wa kundi la BRICS kwa njia ya mawasiliano ya Intaneti

 

Raisi ameongeza kuwa: Iran inazitaka nchi wanachama wa kundi la BRICS kusimama kidete kudumisha usalama na kusimamisha uadilifu na kupambana na ubaguzi wa rangi duniani na kutumia uwezo wao wote wa kisiasa na kiuchumi kuuwekea mashinikizo utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wa Magharibi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na nchi za Magharibi kwa mauaji ya halaiki na mauaji ya watoto wachanga huko Gaza kuwa mbaya zaidi kuliko kitu chochote na akasisitiza: Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa hutuma kila aina ya silaha na mabomu kwa utawala wa Kizayuni kila siku na kupinga usitishaji vita. Marekani hata Imefunga njia zote za misaada kuelekea Gaza na kudumaza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.