-
Rais wa Iran: Biden amekiri kwamba Israel ni utawala bandia
Oct 23, 2023 04:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran ameyataja matamshi yaliyotolewa na Rais wa Marekani, Joe Biden, kuwa yanapinga maendeleo ya kisaisa na kijamii na demokrasia na ni dhidi ya binadamu na akasema: Matamshi ya hivi majuzi ya Rais wa Marekani ni kukiri bila hiari kwamba utawala ghasibu wa Israel ni utawala bandia.
-
Rais Raisi: Hakuna matumaini tena kwa Baraza la Usalama la UN kutekeleza jukumu la kulinda amani ya dunia
Oct 22, 2023 23:32Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini kuwa, hakuna matumaini tena kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza jukumu lake la kulinda amani ya dunia.
-
Amir Abdollahian: Walimwengu wanashuhudia jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza
Oct 22, 2023 11:30Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini kwamba: Hii leo dunia inashuhudia jinai zinazofanywa na utawala wa kibaguzi na muuaji wa watoto wachanga dhidi ya watu wa Gaza.
-
Iran: Hatua za makundi ya Muqawama ya Palestina dhidi ya uvamizi zinaendana na sheria za kimataifa
Oct 22, 2023 03:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Luxembourg kwamba: hatua zinazochukuliwa na makundi ya Muqawama wa Palestina kwa ajili ya kukabiliana na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel zinaendana na sheria za kimataifa.
-
Kan'ani: Kushtakiwa watenda jinai wa Kizayuni ni takwa la wapigania uadilifu duniani
Oct 21, 2023 09:36Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusema kuwa, kushtakiwa watenda jinai wa Kizayuni ni takwa la wapigania uadilifu kote duniani.
-
"Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linakumbusha tabia za ISIS"
Oct 21, 2023 04:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulizi la Israel dhidi ya Kanisa la Saint Porphyrius katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, "Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linashabihiana na nyendo za kundi la kigaidi la ISIS."
-
Afisa wa Iran: Kutayarisha mkataba wa kisheria ndio njia bora ya kuimarisha amani na usalama kimataifa
Oct 21, 2023 03:15Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Amani ya Kimataifa na Usalama katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Kutayarishwa mkataba wa kisheria na kiutendaji ni suluhisho bora zaidi la kuimarisha amani na usalama wa kimataifa.
-
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria: Kimbunga cha Al-Aqsa ni mwanzo wa kushindwa utawala wa Kizayuni
Oct 20, 2023 10:20Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (NIM) amesisitiza kuwa: operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni mwanzo wa kushindwa na kurudi nyuma jeshi lenye nguvu bandia la utawala wa Kizayuni.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Shambulio la Muqawama lililofanywa wakati mwafaka ni halali na linakubalika kimataifa
Oct 20, 2023 10:03Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa, shambulio liliofanywa wakati mwafaka la Muqawama ni halali na linakubalika katika uga wa kimataifa na dhamiri za umma; na halina pingamizi yoyote.
-
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latangaza rasmi kumalizika vikwazo dhidi ya Iran
Oct 19, 2023 23:29Sekretarieti ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imezitumia barua nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa na kuwajulisha rasmi kumalizika vikwazo vya umoja huo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.