-
Raisi: Veto ya US katika Baraza la Usalama ni 'dhulma maradufu' kwa Wapalestina
Oct 19, 2023 11:41Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Marekani ya kulipigia kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusimamishwa mashambulizi na jinai za Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza ni dhulma maradufu dhidi ya Wapalestina na ubinadamu.
-
Abdollahian: Tunataraji kuona uhalifu wa kivita dhidi ya Gaza ukikomeshwa haraka
Oct 19, 2023 10:44Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, tunataraji kuona uhalifu wa kivita dhidi ya Gaza ukikomeshwa haraka iwezekanavyo.
-
Iran: Kuna udharura wa kupandishwa kizimbani viongozi wote wa utawala wa Kizayuni
Oct 19, 2023 02:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuna udharura wa kupandishwa kizimbani viongozi wa utawala wa Kizayuni kutokana na jinai za kuchupa mipaka wanazozifanya dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
-
Iran na Tunisia zafanya mazungumzo ya namna ya kuwasaidia wananchi wa Ghaza
Oct 19, 2023 02:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Tunisia mjini Jeddah, Saudi Arabia na pande mbili zimejadiliana njia za kuwasaidia wananchi wa Ghaza na kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Kumalizika muda wa vikwazo vya makombora dhidi ya Iran
Oct 19, 2023 01:09Tarehe 18 Oktoba 2023 vikwazo vya makombora dhidi ya Iran vilimalizika kwa mujibu wa Azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Baada ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kutangazwa Juni 2015, iliamuliwa kuwa vikwazo vya silaha vya Iran vitamalizika baada ya miaka 5, yaani Oktoba 2020, na vikwazo vya makombora vitamalizika baada ya miaka 8 yaani Oktoba 2023.
-
Rais Raisi: Kila tone la damu ya Wapalestina ni hatua moja mbele kuelekea kuangamia Israel
Oct 18, 2023 22:59Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwenye mjumuiko mkubwa wa wananchi wa Tehran uliofanyika kwa ajili ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni, kwamba, kila tone la damu za Wapalestina zinazomwagwa na Israel ni hatua moja mbele kuelekea kwenye kusambaratika Wazayuni.
-
Muda wa vikwazo kwa makombora ya balestiki ya Iran umemalizika
Oct 18, 2023 22:56Vikwazo kwa mradi wa makombora ya balestiki ya Iran vilivyokuwa vimewekwa na Umoja wa Ulaya vilifikia kikomo Jumatano ya jana Oktoba 18, chini ya Azimio Nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo liliidhinisha mkataba wa nyuklia wa JCPOA wa mwaka 2015.
-
Mamia ya maelfu ya wananchi wa Iran waandamana kote nchini kulaani jinai za Israel
Oct 18, 2023 11:18Mamia ya maelfu ya wananchi Waislamu wa Iran leoJumatano wameandamana katika kona zote za humu nchini kulaani jinai za utawala wa Kizayuni na pia kutangazaa uunaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina.
-
Abdollahian alaani jinai za Israel Gaza: Muda wa utawala wa Kizayuni umemalizika
Oct 18, 2023 08:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kitendo cha Israel cha kushambulia kwa mabomu hospitali na shule katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kueleza kuwa: Muda wa kubaki hai utawala wa Kizayuni umemalizika.
-
Onyo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu kuendelea jinai za Wazayuni
Oct 18, 2023 04:27Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia ulazima wa kusitishwa mashambulizi na jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.