Iran: Kuna udharura wa kupandishwa kizimbani viongozi wote wa utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103670-iran_kuna_udharura_wa_kupandishwa_kizimbani_viongozi_wote_wa_utawala_wa_kizayuni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuna udharura wa kupandishwa kizimbani viongozi wa utawala wa Kizayuni kutokana na jinai za kuchupa mipaka wanazozifanya dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2023 02:37 UTC
  • Iran: Kuna udharura wa kupandishwa kizimbani viongozi wote wa utawala wa Kizayuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuna udharura wa kupandishwa kizimbani viongozi wa utawala wa Kizayuni kutokana na jinai za kuchupa mipaka wanazozifanya dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.

Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo kwenye kikao cha kamati ya utendaji cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC mjini Jeddah Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, kuna wajibu pia wa kuwekewa vikwazo vya kisiasa na kiuchumi viongozi wa utawala wa Kizayuni.

Katika siku za hivi karibuni, jinai za utawala wa Kizayuni zimepindukia mpaka. Juzi Jumanne usiku, jinai za Israel zilifikia kiwango cha kutisha baada ya makatili hao kuua kwa umati mamia ya Wapalestina katika hospitali ya al Maamadani, katikati ya Ukanda wa Ghaza bila ya kujali wagonjwa, watoto wadogo, wanawake, raia wa kawaida wala chochote.

Zaidi ya watu 500 wameuliwa kwa umati na kwa mkupuo mmoja katika shambulio hilo la kikatili lililofanywa Jumanne usiku na wanajeshi makatili wa Israel ambao wameshindwa kwenye medani ya vita na wanamapambano wa Palestina. 

Kabla ya hapo pia utawala wa Kizayuni ulikuwa umeshafanya ukatili mkubwa dhidi ya wananchi wa Ghaza kwa kuua shahidi zaidi ya Wapalestina 3,000, na kujeruhi na kuwafanya wakimbizi maelfu ya Wapalestina wengine. Jinai zote hizo za Wazayuni zinafanyika sambamba na kuzingirwa kila upande Ukanda wa Ghaza na kukatiwa maji, umeme, chakula, madawa na kila kitu cha dharura anachohitaji kila mwanadamu kwa ajili ya kuweza kuishi.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akisema pia kwenye kikao hicho cha mjini Jeddah kwamba Marekani inafanya njama za kuubakisha hai utawala uliosambaratika wa Kizayuni kupitia kufanya mauaji dhidi ya raia wasio na hatia na kwamba Marekani ni mshirika wa moja kwa moja wa jinai za Israel huko Ghaza na Palestina kiujumla.