-
Barua ya Iran kwa taasisi za haki za binadamu za UN kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni
Oct 18, 2023 03:20Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Baraza la Haki za Binadamu na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu na kutaka kusitishwa mashambulizi na jinai za utawala wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Abdollahian: Sera za Marekani zinachochea moto wa vita Gaza
Oct 17, 2023 10:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sera haribifu za Washington na uungaji mkono wake kwa hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuwashambulia raia katika Ukanda wa Gaza ndiyo sababu kuu ya kushadidi na kupanuka vita katika eneo hilo la pwani ambalo liko chini ya mzingiro.
-
Kiongozi Mkuu wa Iran: Jinai za Gaza zisiposimamishwa, hakuna atakayeweza kuwazuia Waislamu na Wanamuqawama
Oct 17, 2023 08:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: wananchi wa mataifa ya Kiislamu na hata watu wasio Waislamu duniani wamekasirishwa sana na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala unaoikalia Quds kwa mabavu, na iwapo unyama na ushenzi huo utaendelea Waislamu duniani na vikosi vya Muqawama wataishiwa na subira na hakuna atakayeweza kuwazuia.
-
Safari ya kieneo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
Oct 17, 2023 02:42Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye amezitembelea nchi nne za Kiarabu za eneo la Asia Magharibi akiongoza ujumbe wa kisiasa kufuatia matukio ya hivi karibuni ya Palestina, amerejea mjini Tehran baada ya kushauriana na viongozi wa nchi hizo na vilevile baadhi ya viongozi wa harakati za mapambano ya ukumbozi wa Palestina.
-
Iran: Kutanuka vita vya Ghaza nje ya mipaka ya Palestina ni jambo lisiloepukika
Oct 17, 2023 02:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, iwapo fursa chache na kidogo sana zilizopo kwenye Umoja wa Mataifa hazitatumiwa vizuri, basi kutanuka vita vya Ghaza nje ya mipaka ya Palestina litakuwa ni jambo lisiloepukika.
-
Raisi amwambia Erdogan: Kila sekunde ni muhimu katika kukomesha jinai za Wazayuni huko Gaza.
Oct 17, 2023 00:20Katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Uturuki, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kila sekunde ni muhimu katika juhudi za kusitisha jinai zinazofanywa na Wazayuni huko Gaza.
-
Meja Jenerali Salami: Kimbunga cha Al Aqsa ni awamu ya kwanza ya kusambaratika utawala wa Kizayuni
Oct 17, 2023 00:16Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amezungumzia oparesheni ya kishujaa ya Kimbunga cha al Aqsa na kusema kuwa oparesheni hiyo ni hatua ya kwanza ya kusambaratika mapema utawala bandia wa Israel.
-
Velayati: Kusimama kidete muqawama ndio njia sahihi ya kufikia kilele cha ushindi
Oct 16, 2023 10:16Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, kusimama kidete muqawama ndio njia sahihi ya kufikia kilele cha ushindi.
-
Kan'ani: Hivi haki za binadamu zinajumuisha pia Palestina?
Oct 16, 2023 10:11Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameihutubu jamii ya kimataifa na kuiuliza, hivi haki za binadamu zinajumuisha pia Palestina?
-
Iran kushiriki kikao cha dharura cha OIC cha mjini Jeddan cha kujadili kadhia ya Palestina
Oct 16, 2023 03:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itashiriki vilivyo katika kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kitakachofanyika mjini Jeddah, Saudi Arabia.