-
Raisi: Inapasa kuwabebesha dhima wanaonyamazia kimya jinai za Israel
Oct 15, 2023 23:38Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina ni katika misingi ya sera za Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, wanaonyamazia kimya jinai za Israel watabeba mas'ulia mbele ya Mwenyezi Mungu, mienendo yao na historia.
-
Abdollahian: Kuendelea mashambulizi ya Israel huko Gaza yumkini kukapanua wigo wa mapigano
Oct 15, 2023 11:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake na Amir Qatar kwamba: "Iwapo mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina na watu wasio na ulinzi katika ukanda wa Gaza yataendelea, hakuna mtu anayeweza kudhibiti hali hiyo au kutoa dhamana na kutopanuka zaidi migogoro huo."
-
Rais wa Iran: Ikiwa mauaji ya watu wa Gaza hayatasitishwa, vita vitaenea
Oct 15, 2023 11:48Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo na Rais wa Ufaransa kuwa, ikiwa jinai za utawala wa Kizayuni ikiwemo mauaji ya raia na kuuzingira Ukanda wa Ghaza hayatasitishwa, hali ya mambo itakuwa tete zaidi na vita vitaenea.
-
Ofisi ya Iran UN: Jinai za Israel zisipositishwa, huenda hali haitaweza kudhibitika tena
Oct 15, 2023 04:11Ofisi ya Uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imetahadharisha kuwa iwapo jinai na uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa kibaguzi wa apathaidi wa Israel hayatakomeshwa mara moja, huenda hali haitaweza kudhibitika tena.
-
Ebrahim Raisi: Kimbunga cha al-Aqswa ni upanga uliotolewa katika ala yake baada ya kushadidi jinai za Wazayuni
Oct 15, 2023 00:06Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Kimbunga cha al-Aqswa ni upanga uliotolewa katika ala yake baada ya kushadidi jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kiongozi Muadhamu aonana na Sheikh Zakzaky, asema Palestina ni dhihirisho la nguvu za Uislamu
Oct 14, 2023 10:30Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonana na Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kusisitiza kuwa, Palestina na Ghaza ni dhihirisho la nguvu za Uislamu.
-
Iran yakosoa taarifa ya Arab League kuhusu Gaza
Oct 14, 2023 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taarifa mpya ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu juu ya matukio ya Ukanda wa Gaza inakera na kufedhehesha.
-
Meja Jenerali Salami: Kimbunga cha Al-Aqswa ni ushindi mkubwa zaidi wa harakati ya Palestina
Oct 13, 2023 23:32Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, kipigo kikubwa zaidi katika historia ya uwepo wa utawala bandia wa Kizayuni tangu mwaka 1948 kwa utawala huo na ushindi mkubwa zaidi wa harakati ya Palestina ulitokea katika operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Kuongezeka Waislamu wanaounga mkono muqawama wa Palestina ni dhihirisho la Mwamko wa Kiislamu
Oct 13, 2023 08:41Khatibu wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Tehran amesema kuwa kujitokeza wimbi kubwa na uungaji mkono wa Waislamu katika maeneo mbalimbali duniani kwa mapambano ya wananchi wa Palestina ni jambo lenye baraka na la kusifiwa linalodhihirisha mwamko wa Kiislamu.
-
Azimio la mwisho katika maandamano ya Iran ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni
Oct 13, 2023 08:30Washiriki wa maandamano ya leo hapa nchini ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wamewasilisha azimio mwishoni mwa maandamano hayo na kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi madhlumu wa Palestina.