Iran yakosoa taarifa ya Arab League kuhusu Gaza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taarifa mpya ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu juu ya matukio ya Ukanda wa Gaza inakera na kufedhehesha.
Hossein Amir-Abdollahian alisema hiyo jana Ijumaa katika kikao na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Lebanon, Faisal Mekdad huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon, kikiwa ni kituo cha pili cha ziara yake ya kieneo, baada ya kuitembelea Iraq.
Amesema taarifa hiyo ya Arab League haiakisi mitazamo ya mawaziri wote wa mambo ya nje wa nchi za Kiislamu na kusisitiza kuwa, Iran, Iraq na nchi nyingine katika eneo zinaunga mkono kufanyika kwa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislami OIC.
Mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wasio na ulinzi wa eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kwa mabavu yangali yanaendelea. Wapalestina zaidi ya 1,500 wameuawa shahidi mpaka sasa, mbali na wengine zaidi ya 6,000 kujeruhiwa, huku utawala katili wa Israel ukiendelea kuwashambulia kwa mabomu na makombora Wapalestina wa Gaza.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amesisitiza kuwa, wananchi wa Palestina wana haki ya kisheria ya kujihami dhidi ya aina yoyote ya uchokozi na kukaliwa ardhi zao kwa mabavu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, utawala unaoua watoto wa Kizayuni tayari ulikuwa umeshaua watoto zaidi ya 50 wa Kipalestina, tangu kuanza mwaka huu, hadi kabla ya kufanyika Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon, Faisal Mekdad amesema ni wazi kuna hali ya kutoelewana miongoni mwa mataifa ya Kiarabu, lakini taarifa ya Arab League haiwezi kuzuia nchi za Kiarabu kuwanga mkono Wapalestina.