Velayati: Kusimama kidete muqawama ndio njia sahihi ya kufikia kilele cha ushindi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103560-velayati_kusimama_kidete_muqawama_ndio_njia_sahihi_ya_kufikia_kilele_cha_ushindi
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, kusimama kidete muqawama ndio njia sahihi ya kufikia kilele cha ushindi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 16, 2023 10:16 UTC
  • Velayati: Kusimama kidete muqawama ndio njia sahihi ya kufikia kilele cha ushindi

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, kusimama kidete muqawama ndio njia sahihi ya kufikia kilele cha ushindi.

Dr. Ali Akbar Velayati mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjinii Tehran na mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ambapo ametoa pongezi pia kwa muqawama wa Palestina kufuatia ushindi wao dhidi ya adui mzayuni.

Akizungumza na Khalid Qaddoumi ambaye ni mwakilishi wa Harakati ya Hamas mjini Tehran, Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Masuala ya Kimataifa amesema: Kasi ya uchukuaji hatua katika kile kilichofanyika inastaajabisha sana na ni kitendo kikubwa kilichowashangaza maadui.

Velayati ameongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko pamoja na watu wanaodhulumiwa wa Palestina na tutaendelea na uungaji mkono wetu wa kimaanawi.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu katika masuala ya kimataifa pia amesema: Leo ulimwengu wa Kiislamu umeungana katika kuiunga mkono Palestina.

Khalid Qaddoumi mwakilishi wa Harakati ya Hamas mjini Tehran

 

Velayati ameongeza kuwa: Utawala ghasibu wa Israel umo katika hali ya kuangamia na taifa la Palestina litaendelea kuwa na fahari na ushindi.

Aidha amebainisha pia kwamba, tunaitambua Palestina kuwa iko katika kitovu cha mapambano dhidi ya dhalimu, na yeyote mwenye msimamo thabiti huko Palestina maana yake ni mtu thabiti katika njia ya Uislamu.

Kwa upande wake, Khalid Qaddoumi, mwakilishi wa Hamas nchini Iran sambamba na kuthamini misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono malengo matukufu ya taifa la Palestina amesisitiza kuwa: Licha ya mafanikio na ushindi wote uliopatikana, lakini mafanikio na ushindi wa hivi karibuni wa taifa la Palestina haukuwa na mithili na wananchi wa Palestina wamethibitisha kuwa utawala wa Kizayuni unazidi kudidimia, na tutaikomboa Quds tukufu kutoka katika makucha ya Wazayuni maghasibu.