"Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linakumbusha tabia za ISIS"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103748-shambulio_la_israel_dhidi_ya_kanisa_gaza_linakumbusha_tabia_za_isis
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulizi la Israel dhidi ya Kanisa la Saint Porphyrius katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, "Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linashabihiana na nyendo za kundi la kigaidi la ISIS."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 21, 2023 04:10 UTC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulizi la Israel dhidi ya Kanisa la Saint Porphyrius katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, "Shambulio la Israel dhidi ya kanisa Gaza linashabihiana na nyendo za kundi la kigaidi la ISIS."

Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo kwenye ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa X (Twitter) na kuongeza kuwa: Tabia ya kinyama ya utawala huu unaochukiwa, ya uvamizi, kuvunjia heshima matukufu ya kidini, na kushambulia turathi za kihistoria na utamaduni wa mwanadamu, inafanana na ya makundi ya kutisha ya kigaidi kama ISIS.

Juzi Alkhamisi, Wakristo wasiopungua 18 wa Kipalestina waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la anga la Israel lililolenga Kanisa hilo la Kiothodoksi la Ugiriki katika Ukanda wa Gaza.

Kanisa la Saint Porphyrius linalohesabiwa kuwa moja ya makanisa makongwe zaidi katika eneo, linapatikana katika eneo la Zeitoun, kusini mwa Gaza, yapata mita 250 kutoka Hospitali ya Kibaptisti ya Al Alhli Arab, lililoshambuliwa na Wazayuni siku chache zilizopita.

Jumanne usiku, jinai za Israel zilifikia kiwango cha kutisha baada ya makatili hao kuua kwa umati mamia ya Wapalestina katika hospitali hiyo ya al Maamadani, katikati ya Ukanda wa Gaza bila ya kujali wagonjwa, watoto wadogo, wanawake, raia wa kawaida wala chochote.

Zaidi ya watu 500 waliuliwa kwa umati na kwa mkupuo mmoja katika shambulio hilo la kikatili lililofanywa Jumanne usiku na wanajeshi makatili wa Israel ambao wameshindwa kwenye medani ya vita na wanamapambano wa Palestina. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, mienendo hiyo ya Israel ya kushambulia makanisa na hospitali katika Ukanda wa Gaza haitofautiana na ya ISIS.