-
Raisi aitaka jamii ya kimataifa isimamishe jinai za Israel Ukanda Gaza
Oct 11, 2023 23:03Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameikumbusha jamii ya kimataifa kuwa ina wajibu wa kukomesha mgogoro katika wa Ukanda wa Gaza, ambapo Wapalestina wa eneo hilo wanakabililiwa na kila aina ya jinai kutoka kwa Wazayuni.
-
Gadi za pwani za Iran zafanya mazoezi makubwa ya kijeshi fukwe za kusini
Oct 11, 2023 09:15Gadi za Pwani za Iran zimeanza mazoezi makubwa ya kijeshi katika fukwe za Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman na kaskazini ya Bahari Hindi.
-
Kan'ani: Sauti ya Kushindwa Wazayuni imesikiwa na walimwengu
Oct 11, 2023 09:07Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya waandishi wa habari hayatazuia kufichuliwa ukubwa wa kushindwa kwa utawala huo na jinai zake na kuongeza kuwa: Msingi unaolegalega wa utawala dhalimu na bandia wa Israel unatetereka zaidi, na sauti za kufeli na kushindwa kwake kijeshi na kijasusi imefika kwenye masikio ya walimwengu.
-
Zakzaky akiwa Tehran: Mapinduzi ya Kiislamu yataleta mabadiliko duniani
Oct 11, 2023 08:39Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) amesema anatumai Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yataleta mabadiliko na mageuzi katika kona zote za dunia.
-
Muirani aliyevumbua dawa dhidi ya saratani atunukiwa medali ya dhahabu ya dunia
Oct 11, 2023 04:25Mvumbuzi Muirani aliyevumbua dawa ya kuzuia ugonjwa wa saratani (cancer) ametunukiwa medali ya dhahabu katika Mashindano ya Kimataifa ya Uvumbuzi na Ubunifu ya Uswisi ya mwaka 2023.
-
Iran: Wapalestina wana haki kisheria ya kujihami na uvamizi na kukaliwa ardhi zao na Israel
Oct 10, 2023 23:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akieleza wasiwasi alionao kuhusu hujuma na jinai za kutisha zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel, na kusisitiza kwamba wananchi wa Palestina wana haki ya kisheria ya kujihami dhidi ya aina yoyote ya uchokozi na kukaliwa ardhi zao kwa mabavu.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Israel itachapwa "kibao kikali zaidi" kwa mauaji ya halaiki inayofanya Ukanda wa Gaza
Oct 10, 2023 11:08Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Israel itachapwa "kibao kikali zaidi" kwa mauaji inayoendelea kufanya dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza iliouwekea mzingiro.
-
Iran: Tuko tayari kuongoza mkutano wa nchi za Kiislamu kujadili Palestina
Oct 10, 2023 10:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ipo tayari kuwa mwenyeji wa mkutano wa dharura wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), kwa ajili ya kuzungumzia kadhia ya Palestina.
-
Mtazamo wa kiongozi Muadhamu: Unapodhulumu, subiri kimbunga
Oct 10, 2023 09:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amezungumzia kushindwa "kusikoweza kukarabatiwa" kwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa ya vijana wa Kipalestina.
-
Uungaji mkono wa Iran kwa haki ya kisheria ya kujitetea taifa la Palestina
Oct 10, 2023 04:17Akizungumza kwa nyakati tofauti kupitia mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami pamoja na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas, kuhusu matukio ya hivi karibuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na maghasibu wa Kizayuni, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unazidi kudhoofika na kudidimia na mrengo wa mapambano kuelekea kwenye kilele cha ushindi.