-
Jeshi la Iran la IRGC lasema litazindua zana za kivita zitakazomshangaza adui
Apr 23, 2026 10:59Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kuwa liko tayari kutangaza mafanikio mapya pamoja na zana za kushangaza za kivita zinazozidi upeo wa kuelewa wa adui, likionya kuwa kila kitendo kipya cha uchokozi kitapata majibu makali.
-
Iran Yalalamikia Matumizi Mabaya ya Ardhi na Anga ya Nchi 5 na Marekani
Apr 23, 2026 10:56Amir Saeed Iravani, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa, katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, ametoa malalamiko makali kuhusu matumizi mabaya ya Marekani ya ardhi na anga ya nchi tano za eneo katika hujuma za kijeshi dhidi ya Iran. Nchi hizo ambazo zimeafiki ardhi zao kutumiwa kuishambulia Iran ni pamoja na Qatar, Kuwait, Bahrain, Falme za Kiarabu (UAE) na Saudi Arabia.
-
Araghchi: Mzingiro wa bandari za Iran ni uvunjaji wa makubaliano ya usitishaji vita
Apr 23, 2026 10:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ametoa tamko kufuatia shambulio la Marekani dhidi ya meli ya kibiashara ya Iran katika Bahari ya Oman, akisema kwamba kuweka mzingiro dhidi ya bandari za Iran ni uvunjaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Baqaei: Iran Iko tayari kujilinda mkabala wa vitisho vya adui
Apr 23, 2026 09:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza utayari wa Tehran kujilinda dhidi ya mashambulizi na vitisho vya aina yoyote vya adui.
-
Araqchi: Mashambulizi dhidi ya Iran ni chanzo cha ukosefu wa usalama katika Ghuba ya Uajemi
Apr 23, 2026 09:35Mwakilishi Maalumu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, ambaye aliwasili Tehran kwa ajili ya mashauriano na viongozi wa Iran, amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.
-
Kiongozi Muadhamu awashukuru Maulamaa wa Kisunni wa Hormozgan
Apr 21, 2026 09:19Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, ameelezea shukrani zake za dhati kwa wanazuoni na maulamaa wa Kisunni katika mkoa wa kusini mwa Iran wa Hormozgan, akisifu mshikamano wao na tamko lao la kutoa Bay’a yaani kiapo cha utii.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa vitisho vipya vya Trump dhidi ya Iran
Apr 21, 2026 09:11Msemaji wa Umoja wa Mataifa amekosoa wazi vitisho vipya vya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu kushambulia miundombinu ya Iran endapo matakwa ya Washington hayatatekelezwa.
-
Qalibaf: Hakuna mazungumzo chini ya vitisho, Iran iko tayari kufichua kadi mpya uwanjani
Apr 21, 2026 08:51Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema Tehran haitakubali kufanya mazungumzo na Washington chini ya kivuli cha vitisho.
-
Siku ya Jeshi: Kiongozi apongeza jeshi la Iran kwa ujasiri katika kulilinda taifa dhidi ya wavamizi
Apr 19, 2026 10:57Katika ujumbe alioutoa Jumapili kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei amelisifu Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusimama kwa ujasiri kulilinda taifa katika vita vya hivi karibuni vya kulazimishwa, kama lilivyofanya katika vita vya kulazimishwa vya awamu zilizopita.
-
Iran kudhibiti trafiki ya Lango Bahari la Hormuz hadi makubaliano yafikiwe kumaliza vita
Apr 19, 2026 10:50Baraza la Juu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) limesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kusimamia na kudhibiti trafiki yote inayopita katika Lango Bahari la Hormuz, ambalo ni njia ya kimkakati, hadi kufikiwa mapatano kamili ya kumaliza vita vya kulazimishwa vya Marekani na Israel dhidi ya nchi hii.