-
Umuhimu wa kisiasa wa ibada ya Hija katika maneno ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
May 18, 2023 05:50Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asubuhi ya jana Jumatano (tarehe 17 Mei) alieleza baadhi ya vipengee umuhimu vya kisiasa vya ibada ya Hija katika kikao chake na maafisa, wasimamizi na baadhi ya Wairani waliojiandikisha kushiriki ibada ya Hija mwaka huu.
-
Msafara wa Meli za Kivita za Iran wakamilisha kwa mafanikio safari ya kuzunguka dunia
May 18, 2023 02:35Msafara wa 86 wa Meli za Kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umerejea nchini baada ya safari ya kuzunguka dunia kama sehemu ya juhudi za Jamhuri ya Kiislamu za kupanua uwepo wake kijeshi katika bahari za mbali.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Hija ni mkutano wa kimataifa na miadi ya dunia
May 17, 2023 08:27Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika kikao cha maafisa wanaoshughulikia ibada ya Hija kwamba: Hija ni tukio la kimataifa na miadi ya dunia yenye manufaa mengi ya dunia na Akhera.
-
Kupiga hatua sekta ya mafuta ya Iran licha ya kuandamwa kwa vikwazo
May 16, 2023 21:56Taasisi ya utafiti ya Marekani imetangaza kuwa, takribani kilomita 1900 za mabomba ya mafuta nchini Iran zipo katika hali ya kujengwa na kwamba, licha ya Iran kuandamwa na vikwazo inashika nafasi ya kwanza duniani katika uga huu.
-
Rais wa Pakistan: Maridhiano kati ya Iran na Saudia yatabakia katika historia
May 16, 2023 10:49Rais Arif Alvi wa Pakistan Arif Alvi amepongeza hekima ya Iran na Saudi Arabia ya kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia baina yao akisema kuwa, makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya nchi hizo mbili yatabakia katika historia.
-
Iran: Nchi za Magharibi zimegeuzwa 'pepo ya usalama' kwa magenge ya kigaidi
May 16, 2023 03:33Katibu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Iran amesema nchi za Magharibi ni 'pepo ya usalama' kwa makundi ya kigaidi.
-
Ayatullah Arafi: Dini zote zisimame imara kukabiliana na dhulma za utawala wa Kizayuni wa Israel
May 15, 2023 03:30Mkuu wa vyuo vya kidini nchini Iran amesema: dini zote zinapaswa kusimama imara na kupinga dhulma na ukandamizaji wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Kamanda: Marekani ilishindwa kuuzuia msafara wa manowari za Iran kuvuka Mfereji wa Panama
May 14, 2023 22:11Kamanda wa jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Naibu Admeri Shahram Irani amesema, Marekani ilishindwa kuzuia kundi la 86 la manowari za Jeshi la Wanamaji la Iran kupita kwenye Mfereji wa Panama.
-
Iran: Tunataraji kuona uhusiano wetu na Misri unafufuliwa kikamilifu
May 14, 2023 22:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza matumaini yake kuwa uhusiiano wa Iran na Misri utafufuliwa kikamilifu kutokana na siasa za nje za serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Kitabu kitaendelea kuwa na nafasi ya juu licha ya kuenea mitandao ya kijamii
May 14, 2023 09:47Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mwishoni mwa kutembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran kwamba, licha ya kuenea sana mitandao ya kijamii, lakini nafasi na umuhimu wa kitabu utaendelea kuwa juu.