-
Kutolewa tena sisitizo na Taliban la kutimiza ahadi yake ya kuheshimu haki ya Iran katika maji ya Mto Helmand
Apr 28, 2023 22:19Naibu msemaji wa serikali ya muda ya Taliban amesema kupatikana haki ya Iran ya kutumia maji ya Mto Helmand ni moja ya vipaumbele vya kundi hilo, jambo ambalo halijatekelezwa licha ya ahadi zilizotolewa na maafisa wa Taliban katika kipindi cha karibu miaka miwili sasa.
-
Kanani: Mwisho wa Nakbat na siku ya uhuru wa Palestina vinakaribia
Apr 28, 2023 07:58Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Mwisho wa Nakbat na siku ya ukombozi wa Palestina umekaribia.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran awashukuru wananchi kwa kushiriki kwa wingi maandamano ya Siku ya Quds
Apr 28, 2023 07:57Imam wa Swala ya Ijumaa wa ya Tehran amesema kwamba wananchi wa Iran walichukua hatua madhubuti na kubwa kuelekea katika kuliwezesha zaidi taifa katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, na ametoa shukrani zake kwa ushiriki mkubwa wa wananchi katika maandamano ya siku hiyo ya kuwaunga mkono mapambano ya ukombozi ya Wapalestina.
-
Kanani Chafi: Iran haimuombi yoyote ruhusa katika kupambana na ugaidi
Apr 28, 2023 03:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu matamshi ya uingiliaji kati ya viongozi wa Ujerumani kuhusu hukumu iliyotolewa hapa nchini dhidi ya kiongozi wa kundi la kigaidi la "Tondar" na kueleza kuwa: Iran haitamuomba yoyote ruhusa katika mapambano yake dhidi ya ugaidi na kutekeleza uadilifu dhidi ya magaidi.
-
Rais wa Pakistan: Iran inastahiki pongezi kwa umuhimu inaoyapa masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu
Apr 27, 2023 10:29Rais wa Pakistan amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi na mchango muhimu katika ushughulikiaji wa masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu hususan Palestina na kukabiliana na uenezaji chuki dhidi ya Uislamu na ametoa wito wa kupanuliwa uhusiano wa kiuchumi na kuongezwa kiwango cha biashara kati ya Islamabad na Tehran.
-
Kamanda: Israel itapata jibu kali ikithubutu kuishambulia Iran
Apr 27, 2023 06:22Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa makombora ya Iran yako tayari kulenga kitovu cha utawala wa Kizayuni wa Israel iwapo utawala huo au nchi yoyote itajaribu kutishia usalma wa anga ya Iran.
-
Iran: Tunapinga kuendelea vita nchini Ukraine
Apr 27, 2023 02:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inapinga vita vya Ukraine na inaunga mkono juhudi za kusimamishwa vita na kurejea usalama na amani nchini humo.
-
Iran yaishauri Marekani kujifunza kutokana na kushindwa kwa aibu katika Jangwa la Tabas mwaka 1980
Apr 26, 2023 23:34Iran imeikumbusha Marekani kushindwa kwake kwa kufedhehesha katika Operesheni ya Eagle Claw katika Jangwa la Tabas mwaka 1980 hapa nchini, na kuishauri Washington ijifunze somo kutokana na uhasama wake wa zaidi ya miongo minne dhidi ya taifa la Iran ambalo limesimama kidete.
-
Iravani: Kimya cha Baraza la Usalama kinashajiisha ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina
Apr 26, 2023 07:49Amir Saeid Iravani, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema: "Inasikitisha kwamba Baraza la Usalama, limedhoofisha maazimio ya Umoja wa Mataifa na kuyafanya yasiwe na ufanisi kutokana na ukimya wake mbele ya ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kulifanya taifa hilo likabiliwe na ukatili endelevu."
-
Amir-Abdollahian: Oman ina ubunifu mzuri kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran
Apr 26, 2023 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, serikali ya Oman ina ubumifu mzuri kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran, ubunifu ambao utasaidia kurejea mazungumzo katika suala hilo.