Kanani: Mwisho wa Nakbat na siku ya uhuru wa Palestina vinakaribia
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Mwisho wa Nakbat na siku ya ukombozi wa Palestina umekaribia.
Nasser Kan'ani ameyasema hayo kwa mnasaba wa siku ya leo ya kukumbuka tukio chungu la kuanzishwa utawala bandia wa Israel katika ardhi ya Palestina.
Kuhusiana na jambo hilo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kana'ni, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter hii leo Ijumaa kuwa: Leo ni siku ya kuasisiwa utawala muovu wa Israel, siku ya kukaliwa kwa mabavu nchi na ardhi ya taifa jingine (Palestina), linayoitwa "Siku ya Nakba."
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa: Kinyume na wanavyosema Wazayuni na waungaji mkono wao wa Kimagharibi, Israel sio dola la kidemokrasia ambalo liliundwa katika ardhi isiyo na taifa, bali ni jeshi linaloikalia kwa mabavu ardhi ya taifa jingine na limeanzisha utawala wa kikaumu na kibaguzi.
Kanani Chafi amesema: Marekani na Ulaya zinapaswa kujionea aibu kwamba zote mbili zilisaidia kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya taifa jingiine, zilishiriki kikamilifu katika uanzishaji wa utawala wa kibaguzi, na zinafumbia macho uhalifu mbaya zaidi dhidi ya binadamu wa utawala huo kwa miaka 75 na kuungana na dhalimu dhidi ya wanaodhulumiwa.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa: Licha ya ukandamizaji wa miaka 75 wa wananchi madhulumu wa Palestina, lakini utawala wa kibaguzi leo hii unasumbuliwa na mifarakano na kunyauka ndani kwa ndani, na vilevile mgogoro wa utambulisho wake bandia; na kipindi cha kumalizika Nakba na uhuru ya wa Palestina kimekaribia.
Wakati huo huo maelfu ya Wayahudi wanaopinga Uzayuni wamefanya maandamana huko Quds inayokaliwa kwa mabavu kwa mnasaba wa Siku ya Nakba na kuasisiwa utawala haramu wa Iisrael. Wayahudi hao wanaopinga sera za kibaguzi za Israel wamechoma moto bendera za utawala huo.