Kamanda: Israel itapata jibu kali ikithubutu kuishambulia Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i96722-kamanda_israel_itapata_jibu_kali_ikithubutu_kuishambulia_iran
Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa makombora ya Iran yako tayari kulenga kitovu cha utawala wa Kizayuni wa Israel iwapo utawala huo au nchi yoyote itajaribu kutishia usalma wa anga ya Iran.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Apr 27, 2023 06:22 UTC
  • Brigedia Jenerali Alireza Sabahi-Fard
    Brigedia Jenerali Alireza Sabahi-Fard

Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa makombora ya Iran yako tayari kulenga kitovu cha utawala wa Kizayuni wa Israel iwapo utawala huo au nchi yoyote itajaribu kutishia usalma wa anga ya Iran.

Katika mahojiano na Televisheni ya Al Alam ya Iran, Brigedia Jenerali Alireza Sabahi-Fard amesema: Waisraeli “hawapaswi hata kufikiria kuivamia  anga tukufu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Bila shaka wanajua wakiamua kufanya kitendo hicho watakumbana na jibu kali ambalo litawafanya kujuta.”

Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran ameongeza kuwa, kikosi hicho ni "nguvu kamili" katika eneo hilo, akitoa mfano wa kujitegemea kikosi hicho katika kutengeneza zana za kijeshi na uwezo wa kuuza nje baada ya kujitosheleza kikamilifu.

Aidha amesema: Tunasimama kwa miguu yetu wenyewe na hatuna utegemezi wowote kwa nchi nyingine kuhusu vifaa vya ulinzi wa anga.

Sabahi-Fard pia alibainisha kuwa vifaa vyote vya ulinzi wa anga vya Iran vimeundwa ndani ya nchi na kwamba  vinatengenezwa na vijana wa Iran.

Mfumo wa kujihami angani wa Iran wa Bavar

"Hapo awali, vifaa vya ulinzi wa anga vilikuwa vichache sana na viliagizwa kutoka nje. Sasa, tumefikia kiwango cha maendeleo ya kiteknolojia na ujuzi katika nyanja ya kuzalisha vifaa vya ulinzi wa anga vinavyotuwezesha kuviuza nje ya nchi,” aliongeza.

Wataalamu na wahandisi wa kijeshi wa Iran katika miaka ya hivi karibuni wamefanya mafanikio ya ajabu katika utengenezaji wa aina mbalimbali za vifaa kijeshi na nchi hii sasa imejitosheleza katika sekt aya ulinzi.

Maafisa wa Iran wameweka wazi kwamba nchi hii haitasita kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa makombora, ambayo ni kwa ajili ya ulinzi, na kwamba uwezo wa ulinzi wa Iran hautafikishwe kwenye meza mazungumzo.