Kanani Chafi: Iran haimuombi yoyote ruhusa katika kupambana na ugaidi
(last modified Fri, 28 Apr 2023 07:08:34 GMT )
Apr 28, 2023 07:08 UTC
  • Nasser Kan'ani
    Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu matamshi ya uingiliaji kati ya viongozi wa Ujerumani kuhusu hukumu iliyotolewa hapa nchini dhidi ya kiongozi wa kundi la kigaidi la "Tondar" na kueleza kuwa: Iran haitamuomba yoyote ruhusa katika mapambano yake dhidi ya ugaidi na kutekeleza uadilifu dhidi ya magaidi.

 Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jaji Mkuu wa Mkoa wa Tehran  ilieleza katika ripoti yake ya Februari 21 mwaka huu kwamba: Baada ya kukamilika uchunguzi faili la kesi ya Jamshid Sharmahd, Mahakama ya Mapinduzi ya Tehran ilimhukumu kifo kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la Tondar kwa kupatikana na hatia za kufanya vitendo mbalimbali vya hujuma na uharibifu nchini, kupanga na kuelekeza vitendo vya kigaidi.  

Kuhusiana na suala hilo, hukumu ya kunyongwa Jamshid Sharmahd, kiongozi wa kundi la kigaidi la Tondar, imethibitishwa katika Mahakama ya Juu hapa nchini kwa kuzingatia kipengee A cha Kifungu cha 469 cha Sheria ya Jinai.   

Jamshid Sharmahd 

Baada ya kutokewa  hukumu dhidi ya kiongozi huyo wa kundi la kigaidi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani aliingilia masuala ya ndani ya Iran akimuunga mkono gaidi huyo.

Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu matamshi hayo ya kukaririwa ya baadhi ya viongozi wa Ujerumani baada ya kuidhinishwa hukumu ya mahakama ya na kisheria kwa gaidi na kiongozi wa kundi la Tondar Jamshid Shahmahd akisema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitamuomba yoyote ruhusa katika mapambano yake dhidi ya ugaidi na kutekeleza uadilifu mkabala wa magaidi na kwamba, kauli za uingiliaji kati na za kijuba za baadhi ya viongozi wa Ujerumani kuhusiana na hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Iran dhidi ya gaidi anayejulikana ni mfano wa wazi wa kuunga mkono ugaidi na kuingilia masuala ya ndani ya Iran. Amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitavumilia uingiliaji wa aina hii.