-
Iran yawatimua wanadiplomasia wawili wa Ujerumani kwa kuingilia masuala ya ndani
Mar 02, 2023 00:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa amri ya kufukuzwa wanadiplomasia wawili wa Ujerumani kutokana na kuingilia masuala ya ndani ya nchi.
-
Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya "Walinzi wa Anga ya Wilaya 1401" yamalizika
Mar 01, 2023 07:52Kamanda wa luteka na mazoezi ya pamoja ya kijeshi ambayo yalikuwa maalumu kwa ajili ya askari wa kulinda anga ya Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ametangaza habari ya kumalizika maneva hayo yaliyofanyika chini ya kaulimbiu ya "Walinzi wa Anga ya Wilaya 1401."
-
Eslami: Faili la masuala yanayozozaniwa baina ya Iran na IAEA limeshafungwa
Mar 01, 2023 07:36Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesisitiza kuwa, faili la masuala yanayozozaniwa baina ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), limeshafungwa tayari.
-
Iran: Mkwamo wa sasa wa JCPOA ni matunda ya sera ghalati za Marekani
Mar 01, 2023 04:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameikosoa na kuilaumu Marekani kwa kukwamisha mazungumzo ya kujaribu kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ya mwaka 2015.
-
Iran yakaribisha hatua ya Waarabu ya kuhuisha uhusiano na Syria
Feb 28, 2023 23:10Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepongeza hatua ya nchi za Kiarabu ya kuhuisha na kuimarisha uhusiano na Damascus, akisisitiza kuwa mkondo huo mpya wa kurejea mataifa ya Kiarabu nchini Syria unaonyesha kuporomoka kwa njama za nchi za Magharibi.
-
Sisitizo la Iran la ulazima wa kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya amani mzozo wa Ukraine na Russia
Feb 28, 2023 22:48Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, serikali ya Tehran sambamba na kuheshimu mataifa yote mawili ya Ukraine na Russia na kuweko uhusiano mkongwe baina yake na nchi hizo mbili, kwa mara nyingine tena imeonyesha masikitiko yake makubwa iliyonayo kuhusiana na kuendelea vita na mapigano.
-
Brazil yaruhusu manowari za Iran kutia nanga mjini Rio de Janeiro licha ya mashinikizo ya Marekani
Feb 28, 2023 07:02Serikali ya Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil imeruhusu manowari mbili za kivita za Iran kutia nanga mjini Rio de Janeiro, ikipuuza mashinikizo makubwa ya Marekani kuhusu suala hilo.
-
Iran: HRC imegeuzwa kuwa chombo cha siasa za kigeni za nchi chache zinazoongozwa na Marekani
Feb 28, 2023 06:53Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameikosoa vikali Marekani na "nchi nyingine chache" zinazoongozwa na Washington kwa kutumia vibaya suala la haki za binadamu kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kisiasa. Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran aliyasema hayo jana Jumatatu katika hotuba yake kwa kikao cha 52 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko mjini Geneva, Uswisi.
-
Makamu wa Rais wa Iran: Kutanua uhusiano na nchi za Kiafrika ni sera kuu ya Iran
Feb 28, 2023 04:05Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran amekutaja kupanua uhusiano na maingiliano na nchi za Kiafrika hususan Zimbabwe kuwa ni moja ya njia kuu za sera za kigeni za Iran.
-
Kamalvandi: Mkurugenzi Mkuu wa IAEA kutembelea Tehran karibuni hivi
Feb 27, 2023 22:50Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa: "Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, Muhandisi Mohammad Eslami amemwalika rasmi Bw. Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA kuitembelea Iran siku zijazo.