-
Iran yaripoti kuongezeka kwa mauzo ya nje kwa zaidi ya asilimia 12
Feb 27, 2023 04:36Takwimu za Idara ya Forodha wa Irani (IRICA) zinaonyesha kuwa mauzo ya nje yasiyo ya mafuta kutoka nchini yalipanda kwa 12.22% katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.
-
Amir-Abdollahian: Iran daima inakaribisha diplomasia, haijawahi kujitenga na mazungumzo
Feb 27, 2023 04:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema Iran daima imekuwa ikiunga mkono njia ya kidiplomasia ya utatuzi wa hitilafu na haijawahi kujiweka mbali na meza ya mazungumzo.
-
Jen. Salami: Iran inaunda makombora ya kasi ya supasoniki yanayoweza kuangausha satalaiti
Feb 27, 2023 01:27Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema wataalamu katika jeshi hilo sasa wako mbioni kuunda kwa wingi makombora ya kasi ya supasoniki ambayo yana uwezo wa kufuatilia na kutungua hata satalaiti iliyo katika harakati.
-
Iran kuanza kuuza bidhaa za nyuklia nje ya nchi
Feb 26, 2023 08:11Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) ametangaza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inajiandaa kuanza kusafirisha nje ya nchi bidhaa zake za nyuklia, zikiwemo za tiba.
-
Kan'ani: Marekani haina hadhi ya kuzungumza moja kwa moja na Iran kuhusu JCPOA
Feb 25, 2023 23:20Masemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, hakuna udharura wowote wa kuweko mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Iran na Marekani kwa ajili ya kufufuliwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Ameongeza kuwa, serikali ya Marekani haina hadhi ya kuzungumza moja kwa moja na Iran na haiaminiki hata kidogo.
-
Iran yazindua kombora jipya zaidi la Cruise linalofika umbali wa kilomita 1,650
Feb 25, 2023 04:24Kombora la Paveh, ambalo ni kombora jipya zaidi la ardhini la Iran lenye uwezo wa kufika umbali wa kilomita 1,650, limezinduliwa na Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
Raisi: Shahidi Soleimani, IRGC mashujaa wa vita dhidi ya ugaidi
Feb 24, 2023 23:53Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza rekodi ya kuvutia ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika vita dhidi ya ugaidi na kusema kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni nembo na shujaa wa mapambano dhidi ya magenge ya kigaidi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Mahusiano ya pande mbili ya Iran na Iraq; mhimili wa mazungumzo ya Amir-Abdollahian mjini Baghdad
Feb 24, 2023 09:49Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko safarini nchini Iraq amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo Rais na Waziri Mkuu na kujadili uhusiano wa pande mbili na wa kieneo.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran aikosoa Ujerumani kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa Iran
Feb 24, 2023 09:36Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amekosoa hatua ya serikali ya Ujerumani ya kuwafukuza wanadiplomasia wa Iran na kusisitiza ulazima wa kukabiliana ipasavyo na kitendo hicho.
-
Kamalvandi: Shutuma za IAEA dhidi ya Iran 'zimechochewa kisiasa'
Feb 24, 2023 04:29Ripoti zisizoisha za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) zinazotoa shutuma za uwongo na zisizo na msingi dhidi ya mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran "zina msukumo wa kisiasa" ili kuishinikiza nchi hii.