Iran yaripoti kuongezeka kwa mauzo ya nje kwa zaidi ya asilimia 12
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i94512-iran_yaripoti_kuongezeka_kwa_mauzo_ya_nje_kwa_zaidi_ya_asilimia_12
Takwimu za Idara ya Forodha wa Irani (IRICA) zinaonyesha kuwa mauzo ya nje yasiyo ya mafuta kutoka nchini yalipanda kwa 12.22% katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 27, 2023 04:36 UTC
  • Iran yaripoti kuongezeka kwa mauzo ya nje kwa zaidi ya asilimia 12

Takwimu za Idara ya Forodha wa Irani (IRICA) zinaonyesha kuwa mauzo ya nje yasiyo ya mafuta kutoka nchini yalipanda kwa 12.22% katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.

IRICA ilisema katika taarifa yake Jumapili kwamba mauzo ya nje kutoka Iran yalifikia jumla ya dola bilioni 48.8 kati ya Machi 2022 na Februari mwaka huu.

Takwimu hizo hazihusu mauzo ya Iran ya mafuta ghafi ya petroli, na mafuta ya taa pamoja na bidhaa zinazobebwa na abiria.

Taarifa ya IRICA imesema bidhaa za petrokemikali  zilichangia dola bilioni 21.7 sawa na asimilia 44.49 ya mauzo yote ya Iran kati ya Machi mwaka jana na Februari mwaka huu, na kuongeza kuwa Iran imeuza nje gesi aina ya LPG yenye thamani ya dola bilioni 6.8 katika kipindi hicho.

Idara ya Forodha ya Iran imesema China ilikuwa mteja mkubwa zaidi wa mauzo ya nje ya Iran katika kipindi cha miezi 11 hadi mwishoni mwa mwezi Februari ikiwa na manunuzi yenye thamani ya dola bilioni 13.6, ikifuatiwa na Iraq iliyonunua bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 9.4 na Uturuki dola bilioni 6.9.

Benki Kuu ya Iran

Kuhusu uagizaji wa bidhaa kutoka nje, Idara ya Forodha ya Iran imesema kuwa Iran imepokea bidhaa zenye thamani zenye uzito wa tani milioni 33.6 zenye thamani ya dola bilioni 53.7 kati ya Machi mwaka jana na Februari mwaka huu, na kuongeza kuwa takwimu hiyo ni ongezeko la asilimia 15.28 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mafanikio hayo yanajiri pamoja na kuwa madola ya Magharibi yameiwekea Iran vikwazo ili kuzuia biashara ya kimataifa ya Iran. Bidhaa za Iran zinaendelea kupata umaarufu duniani kutokana na viwango bora na bei nafuu.