-
Kiongozi Muadhamu awashukuru wanazuoni wa Kisuni wa Kurdistan kwa uungaji mkono wao
Apr 01, 2026 03:20Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa shukrani kwa wanazuoni wa Kisuni katika Mkoa wa Kurdistan nchini Iran kufuatia ujumbe wao wa pole na mshikamano baada ya kuuawa shahidi aliyekuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
-
Mwakilishi wa Iran UN alaani shambulio la US na Israel dhidi ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Tehran
Apr 01, 2026 03:13Balozi na mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Katibu Mkuu na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo, akilaani mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Tehran na kutoa wito wa ufuatiliaji wa haraka na kutolewa ripoti rasmi kuhusu tukio hilo.
-
Araghchi: Iran haijatoa jibu lolote kwa mapendekezo 15 ya Marekani
Apr 01, 2026 03:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Tehran hadi sasa haijatoa jibu kwa mapendekezo 15 ya Marekani, wala haijawasilisha sharti lolote.
-
Ahadi ya Kweli 4, Wimbi la 88: Jeshi la Wanamaji la IRGC laharibu mfumo wa kukabiliana na droni wa US Fifth Fleet
Mar 31, 2026 06:18Kikosi cha Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mapema leo Jumanne kimefanya operesheni nne dhidi ya shabaha za magaidi wa Kimarekani na Israel na kutoa vipigo vikali ikiwa ni sehemu ya wimbi la 88 la Operesheni Ahadi ya Kweli-4.
-
Pezeshkian alishukuru taifa la Iraq kwa kuwa bega kwa bega na Iran katika mapambano dhidi ya Marekani, Israel
Mar 31, 2026 06:17Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesifu na kupongeza ujasiri wa taifa la Iraq wa kusimama bega kwa bega na watu wa Iran katika kipindi hiki cha uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Mapambano ya Watu wa Iran dhidi ya Madhalimu
Mar 31, 2026 04:51Swali muhimu zaidi ambalo limekuwa likiwashughulisha wachambuzi wengi na hata watumiaji wa mitandao ya kijamii siku hizi ni kuwa: "Je, Wairani wameweza vipi kusimama imara mbele ya nguvu mbili zenye silaha za nyuklia bila kuogopa wala kusalimu amri?"
-
Iran yakanusha kuwepo mazungumzo yoyote na Marekani
Mar 31, 2026 00:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amesisitiza kuwa Tehran haijafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani, na amekanusha madai kwamba Jamhuri ya Kiislamu imekubali mapendekezo ya Washington, akieleza kauli hizo kuwa hazina msingi wowote.
-
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC: Israel izoee “Mfumo Mpya wa Kikanda”
Mar 30, 2026 23:07Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Esmaeil Qaani, amesema kuwa utawala wa Israel unapaswa kuanza kuzoea “mfumo mpya wa nguvu katika kanda y Magharibi mwa Asia,” akisisitiza kwamba hatua zilizoratibiwa na washirika wa Iran katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) zimepunguza kwa kiasi kikubwa matarajio ya usalama ya Israel.
-
Awamu ya pili ya wimbi la 86 la Oparesheni Ahadi ya Kweli-4; ulipizaji kisasi dhidi ya maeneo ya viwanda ya adui
Mar 30, 2026 07:20Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetoa taarifa ikitangaza kuwa jeshi hilo limetekeleza awamu ya pili ya wimbi la 86 la Oparesheni Ahadi ya Kweli-4 dhidi ya kitongoji cha viwanda cha Neot Hovav huko Beersheba kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel).
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu awashukuru wanazuoni wakuu na wananchi wa Iraq
Mar 30, 2026 01:55Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru na kuthamini misimamo ya msingi ya wanazuoni wakuu wa kidini na wananchi wa Iraq.