Kiongozi Muadhamu awashukuru wanazuoni wa Kisuni wa Kurdistan kwa uungaji mkono wao
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa shukrani kwa wanazuoni wa Kisuni katika Mkoa wa Kurdistan nchini Iran kufuatia ujumbe wao wa pole na mshikamano baada ya kuuawa shahidi aliyekuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Katika ujumbe uliotumwa kwa wanazuoni wa Ahlul Sunna wa Kurdistan siku ya Jumanne, Kiongozi Muadhamu amewashukuru kwa salamu zao za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran, akitoa shukrani kwa hisia zao njema walizoonesha kwake.
Sehemu ya ujumbe huo imesomeka: “Wanazuoni waheshimiwa wa Mkoa wa Kurdistan; natoa shukrani kwenu kwa kuotoa kwenu mkono wa pole na salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran, pia nawashukuru kwa wema na upendo mlionionesha mimi binafsi.”.
Ayatullah Khamenei pia amepongeza msimamo “uliowazi na thabiti” wa wanazuoni wakuu wa kidini wa Iraq pamoja na wananchi wa nchi hiyo kuhusu vita vya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Mojtaba Khamenei ameuthamini msimamo wa wazi wa mamlaka ya kidini ya Iraq na taifa hilo kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Aidha aliwaombea dua ya mafanikio endelevu, akimuomba Mwenyezi Mungu awajaalie ustawi na kuwapa nguvu katika kuendelea kuutumikia Uislamu.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la Marekani na Israel lililolenga ofisi yake tarehe 28 Februari, sawa na tarehe 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, siku ya kwanza ya vita vinavyoendelea dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Wanafamilia kadhaa pia waliuawa shahidi katika tukio hilo, akiwemo binti yake, mkwe wake wa kiume, mkwe wake wa kike pamoja na mjukuu wake.
Vikosi vya jeshi la Iran vinaendelea kujibu uchokozi huo kwa kuvurumisha mfululizo wa makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya ngome za kijeshi na kiuchumi utawala wa Kizayuni waIsrael pamoja na vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyonchi za eneo la Asia Magharibi.