Mapambano ya Watu wa Iran dhidi ya Madhalimu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137700-mapambano_ya_watu_wa_iran_dhidi_ya_madhalimu
Swali muhimu zaidi ambalo limekuwa likiwashughulisha wachambuzi wengi na hata watumiaji wa mitandao ya kijamii siku hizi ni kuwa: "Je, Wairani wameweza vipi kusimama imara mbele ya nguvu mbili zenye silaha za nyuklia bila kuogopa wala kusalimu amri?"
(last modified 2026-03-31T08:33:54+00:00 )
Mar 31, 2026 04:51 UTC
  • Mapambano ya Watu wa Iran dhidi ya Madhalimu

Swali muhimu zaidi ambalo limekuwa likiwashughulisha wachambuzi wengi na hata watumiaji wa mitandao ya kijamii siku hizi ni kuwa: "Je, Wairani wameweza vipi kusimama imara mbele ya nguvu mbili zenye silaha za nyuklia bila kuogopa wala kusalimu amri?"

Imekuwaje katika miaka yote 47 ya mashambulizi ya kijeshi, vikwazo vya kiuchumi na hata vita laini, hakuna yeyote aliyeweza kuwashinda?
Ili kujibu maswali haya muhimu, tunapasa kuyatazama kutokea pande mbili: Upande mmoja ni wa imani, na mwingine ni ustaarabu. Kwa mtazamo wa imani, zaidi ya asilimia 99 ya watu wa Iran ni Waislamu wanaofuata madhehebu ya Ahlul-Bayt wa Mtume Muhammad SAW.
Katika imani hii, Mtume Muhammad hakuwa mtume wa kihistoria tu, bali alikuwa mwanzilishi wa njia ambayo lazima iendelezwe. Na waendelezaji wa kweli wa njia hiyo ni Ahlul-Bayt wake, yaani Watu wa Nyumba yake tukufu, kama vile Imam Ali bin Abi Twalib, ambaye kwao wao ni Shahidi wa Haki na Uadilifu. Au kama Imam Hussein bin Ali (AS), ambaye anaitwa Shahidi wa Njia ya Uhuru.

Kwa karne nyingi, Wairani wamekuwa wakijaribu kuoanisha fikra na matendo yao na familia hii tukufu.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) na Ahlul-Bayt zak watoharifu, kifo cha heshima na utukufu ni bora kuliko maisha ya madhila na unyonge, na “kuuawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambayo wanaitambua kuwa ndiyo njia ile ile ya Tauhidi, uadilifu na ubinadamu, ndiyo hadhi na daraja ya juu kabisa.

Makombora ya Iran yakivurumishwa dhidi ya maeneo ya adui

Kwa fikra hii, kushindwa huwa hakuna maana tena kwa Wairani. Kilicho muhimu ni istiqama, kusimama kidete na mapambano katika njia ya ukweli. Ama washinde vita au wauawe shahidi. Na yote mawili ni ushindi kwa Wairani.
Ama kwa mtazamo wa ustaarabu, Wairani daima wamekuwa na moyo wa hamasa. Kama utapitia harakaharaka fasihi na historia ya Iran utaona kwamba muqawama na mapambano dhidi ya uvamizi wa kigeni ni utambulisho wa Kiirani uliokita mizizi.

Kuanzia ushindi wa Wairani kabla ya ujio wa Uislamu dhidi ya Warumi, hadi kushindwa kwa wavamizi baada ya Uislamu, kama vile Wareno na Waingereza, na kilele chake, ni ushindi mkubwa katika vita vya kulazimishwa.
Vita hivyo vilianzishwa na dikteta za zamani wa Iraq, Saddam Hussein dhidi ya Iran kwa msaada wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Umoja wa Kisovieti na nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi, na miaka miwili tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 na kuanzishwa mfumo wa jamhuri badala ya utawala wa kifalme wa Pahlavi.

Hatimaye, Wairani wana ubeti mashuhuri wa shairi ambao umechorwa kwenye akili zao tangu utotoni, unaosema: «چو ایران نباشد تن من مباد!»
"Ikiwa Iran haitakuwepo, basi mwili wangu pia usiwepo!"

Kwa maana kwamba, iwapo italazimu kwamba Iran isiwepo, mimi pia sipaswi kubakia hai!