-
Marais wa Iran na Ufaransa wazungumza kuhusu kupunguza mvutano Asia Magharibi
Mar 25, 2026 04:25Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema kuwa katika mazungumzo ya simu na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, walijadili suala la Lango Bahari la Hormuz na namna ya kupunguza mvutano katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
-
Rais Pezeshkian: Ukosefu wa usalama Lango la Hormuz ni matokeo ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran
Mar 24, 2026 07:53Rais Masoud Pezeshhkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif ambapo pande hizo mbili zimejadili uhusiano wa nchi mbili, matukio ya sasa katika kanda ya Magharibi mwa Asia na athari za vita haramu vya Marekani na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Iran kwa usalama na kanda na dunia nzima.
-
Brigedia Jenerali Rezaei amwambia Trump: Ukipiga miondombinu yetu hatutalipiza kisasi cha jicho kwa jicho, bali kichwa kwa jicho
Mar 24, 2026 07:52Kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza udharura wa kuendelezwa vita hadi Iran itakapolipwa gharama kamili za hasara zilizosababishwa na adui Mmarekani na Mzayuni.
-
Jeshi la Iran: Droni za adui zilizotunguliwa hadi sasa ni 132
Mar 24, 2026 06:49Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuangushwa kwa ndege isiyo na rubani au droni moja ya kivita aina ya Hermes ya utawala haramu wa Israel katika anga ya Tehran mapema Jumanne.
-
Majibu ya Qalibaf kwa madai ya uongo ya Trump: Watu wa Iran wanataka wavamizi waadhibiwe kikamilifu
Mar 24, 2026 05:14Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amejibu madai ya uongo ya rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kuwepo kwa mazungumzo na Iran.
-
Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi: Vita na Iran si filamu ya Hollywood
Mar 23, 2026 07:11Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi Iran ya Khatamul Anbiyaa (SAW) amesema kuiambia Marekani na Israel kwamba: Munafanya makosa kufananisha vita vyenu na taifa lenye ghera na jeshi imara la Iran na filamu za Hollywood na mashujaa za kidhahania na wa kubuni akilini, na mumeanzisha uchokozi kutokana na makosa ya kimahesabu.
-
Qalibaf azitahadharisha taasisi za fedha zinazodhamini bajeti ya kijeshi ya Marekani
Mar 23, 2026 07:03Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezitahadharisha taasisi za fedha zinazodhamini bajeti ya kijeshi ya Marekani.
-
Iran: Dunia imechoshwa na hadithi za uongo za Marekani na Israel
Mar 23, 2026 05:30Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, ameashiria msimamo wa Katibu Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi-NATO- kuhusu kukataa madai ya hivi karibuni ya maafisa wa utawala wa Kizayuni Israel kuhusu tishio la makombora ya Iran kwa Ulaya na kuandika katika mtandao wa X kuwa dunia imechoka na simulizi za uongo za Marekani na Israel.
-
Taarifa ya Ayatullah Hajj Sheikh Muhammad Jawad Fadhil Lankarani, Kuhusu Hatua Isiyofaa ya Al-Azhar
Mar 23, 2026 04:44Katika kujibu hatua ya hivi karibuni ya viongozi wa Al-Azhar, Chuo Kikuu cha Kidini cha nchini Misri ya kulaani hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kulipiza kisasi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani katika ardhi za nchi za Kiarabu za Ghuba ya Ujemi, viongozi tofauti wa kidini akiwemo Ayatullah Sheikh Muhammad Jawad Fadhil Lankarani, wametoa taarifa wakikosoa vikali hatua hiyo ya kibaguzi ya wanazuoni wa Al- Azhar.
-
Mwisho wa makubaliano ya Atlantiki; kwa nini Marekani imetengwa katika vita vyake vya kichokozi dhidi ya Iran?
Mar 22, 2026 07:30Duru ya pili ya hujuma za kijeshi za Marekani na utawala wa Kizayuni imekuwa nukta muhimu katika historia ya mikataba na makubaliano ya kijeshi katika ulimwengu wa Magharibi.