Jeshi la Iran: Droni za adui zilizotunguliwa hadi sasa ni 132
Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuangushwa kwa ndege isiyo na rubani au droni moja ya kivita aina ya Hermes ya utawala haramu wa Israel katika anga ya Tehran mapema Jumanne.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya jumla ya droni za adui zilizoangushwa zikiwa katika anga ya Iran hadi sasa imefikia 132 tokea Februari 28 wakati Marekani na Israel zilipoanzisha vita vya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo ilitekelezwa na mfumo mpya wa kisasa wa ulinzi wa anga wa IRGC, uliokuwa ukifanya kazi chini ya usimamizi wa mtandao jumuishi wa ulinzi wa anga wa taifa.
Juzi pia, Jeshi la Iran lilitangaza kuwa limetungua ndege ya kivita aina ya F15 ya maadui wavamizi, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, kusini mwa nchi.
Ripoti iliyotolewa na Jeshi la Iran ilisema, ndege ya kivita aina ya F15 ya adui ilipigwa kwa kombora katika anga ya maeneo ya pwani kusini mwa Iran, karibu na kisiwa cha Hormuz.
Hiyo ni ndege ya saba ya kivita ya muungano wa Marekani na Israel kutunguliwa na majeshi ya Iran katika vita vya sasa vya tawala hizo mbili dhalimu na vamizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Siku chache zilizopita, ndege ya kivita ya kimkakati aina ya F‑35 ya Jeshi la Marekani ilipigwa kwa kombora na kuharibiwa vibaya ikiwa katika anga ya kati mwa Iran kwa lengo la kutekeleza mashambulizi. Hii ilikuwa mara kwa kwanza katika historia kwa lengo hiyo ya kisasa kabisa kulengwa. Mradi wa kuunda ndege hiyo unakadiriwa kugharimu dola trilioni mbili.
Ndege hiyo ya kisasa ilipigwa kwa mfumo mpya wa kisasa wa ulinzi wa anga wa Kikosi cha Anga cha IRGC katika anga ya Iran ya kati, na kuharibiwa vibaya.
Ndege hizo za adui zilizoangushwa kwa mifumo ya ulinzi ya Iran zimemsababishia adui hasara ya mabilioni ya dola hadi sasa.