Qalibaf azitahadharisha taasisi za fedha zinazodhamini bajeti ya kijeshi ya Marekani
-
Muhammad Baqir Qalibaf
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezitahadharisha taasisi za fedha zinazodhamini bajeti ya kijeshi ya Marekani.
Muhammad Baqir Qalibaf ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akizihutubu taasisi za fedha zinazodhamini bajeti ya kijeshi ya Marekani kwamba: Tunauzingatia mchango wengu; hili ni onyo la mwisho.
Qalibaf ameendelea kuandika: Mbali na kambi za kijeshi, taasisi zote za fedha zinazodhamini bajeti ya kijeshi ya Marekani ni shabaha zetu halali.
Spika Qalibaf pia ametahadharisha kuwa bei ya mafuta duniani itasalia juu kwa muda mrefu iwapo jeshi la Marekani litafanya hujuma yoyote dhidi ya miundo msingi muhimu ya Iran.
Jumatano iliyopita Marekani na Israel zilishambulia baadhi ya visima vya gesi vya Pars-Kusini nchini Iran katika siku ya 19 ya vita vilivyoanzishwa na pande mbili hizo dhidi ya Iran.
Iran ilijibu mapigo kwa kushambulia taasisi na viwanda vya gesi vya makampuni ya Marekani katika nchi mbalimbali za Kiarabu na katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.