-
Rais Raisi: Haiwezekani kufikia makubaliano bila faili la Iran katika IAEA kufungwa
Sep 20, 2022 22:39Rais Ebrahim Raisi amesema, haiwezekani kufikia makubaliano ya nyukllia bila faili la Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kufungwa; na akaongeza kwamba, Ulaya inapaswa ionyeshe kivitendo kuwa sera zake hazina mfungamano na Marekani.
-
Vikwazo, ugaidi, vita na umwagaji damu; matokeo ya uchukuaji maamuzi ya upande mmoja
Sep 20, 2022 09:26Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran adhuhuri ya jana Jumatatu aliwasili mjini New York akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Tehran kwa minajili ya kushiriki katika mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
-
Iran: Vikwazo, ugaidi na vita vya umwagaji damu ndiyo matunda ya siasa za upande mmoja
Sep 20, 2022 04:41Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ammbaye yuko mjini New York Marekani kwa ajili ya kuhutubia Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja a Mataifa amesema kuwa, matunda ya siasa na misimamo ya upande mmoja ya madola ya kibeberu hasa Marekani ni kuongezeka ugaidi na vita vya umwagaji wa damu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.
-
Mazungumzo ya kuondoa vikwazo; ajenda kuu ya mazungumzo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Qatar
Sep 20, 2022 03:36Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar wamezungumzia suala la kuondolewa vikwazo katika fremu ya vikao vya Vienna.
-
Msisitizo mwingine wa Iran wa kuwa tayari kubadilishana wafungwa na Marekani
Sep 19, 2022 21:51Nasser Kanaani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni alitembelea shirika la habari la ISNA ambapo pamoja na mambo mengine alifanyiwa mahojiano maalumu na ripota wa shirika hilo lililopo jijini Tehran.
-
Rais wa Iran: Sina mpango wa kukutana na rais wa Marekani New York
Sep 19, 2022 06:45Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Iran Ebrahim Raisi anasema hana mpango wa kukutana na rais wa Marekani Joe Biden kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
-
Ebrahim Raisi: Wapalestina ndio wenye haki ya kuishi katika ardhi za Palestina
Sep 19, 2022 02:56Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi wa Palestina ndio wenye haki ya kujiamulia wenyewe mustakbali wao na ndio wenye haki ya kuishi katika ardhi hizo.
-
Rais wa Iran leo ameelekea New York kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la UN
Sep 18, 2022 22:25Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi leo Jumatatu ameelekea New York kuhutubia katika kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu kuhusu "mfumo wenye haki wa kimataifa kupitia ushirikiano wa kiuchumi wa pande kadhaa."
-
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mwamko wa Kiislamu Ulimwenguni: Dalili za kuporomoka utawala wa Kizayuni zinazidi kuonekana
Sep 18, 2022 08:32Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mwamko wa Kiislamu Ulimwenguni amewakosoa wale wanaojaribu kuanzisha uhusiano wa kawaida na kuutambua rasmi utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa: Mwenendo wa kihistoria na kudidimia taratibu kwa utawala huo unazidi kuonekana siku baada ya siku.
-
Kanaani: Arubaini ya mwaka huu imeimarisha uhusiano wa Iran na Iraq
Sep 18, 2022 03:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Arubaini ya Imam Hussein (AS) ya mwaka huu imeimarisha uhusiano wa kidugu na kirafiki wa Iran na Iraq.