Sep 18, 2022 08:14 UTC
  • Kanaani: Arubaini ya mwaka huu imeimarisha uhusiano wa Iran na Iraq

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Arubaini ya Imam Hussein (AS) ya mwaka huu imeimarisha uhusiano wa kidugu na kirafiki wa Iran na Iraq.

Huku akiishukuru serikali ya Iraq kwa kuwapokea na kuwa mwenyeji wa mamilioni ya Mazuwari wa Kiirani mwaka huu, Nasser Kanani,  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: Arubaini ya mwaka huu 2022 imetia nguvu uhusiano, udugu na urafiki wa mataifa mawili ya Iran na Iraq.

Amesema kutoshuhudiwa mikusanyiko ya Arubaini miaka miwili iliyopita kutokana na janga la Corona hakujapelekea kuzima moto wa harakati ya matembezi na mkusanyiko huo mkubwa wa kidini mwaka huu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo leo hapa Tehran katika kikao na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, Arubaini ni ni moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani.

Wafanyaziara milioni 20 wamekusanyika katika mji wa Karbala wa Iraq kuadhimisha Arbaeen, tukio la kila mwaka ambalo linaadhimisha siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa madhehebu ya Shia.

Serikali ya Iran ilisema Jumatano kwamba wafanyaziara wa Iran zaidi ya milioni tatu, walimiminika Iraq kushiriki katika kumbukumbu za Arbaeen. 

 

Tags