-
Ghalibaf: Zana za ulinzi za Iran zimewatia kiwewe maadui; wanaogopa kuingia vitani
Aug 27, 2022 20:53Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, zana za ulinzi za Jamhuri ya Kiislamu zimeongeza nguvu za kujihami taifa hili, zimewatia kiwewe maadui na zimewafanya waogope kuingia vitani na Iran ya Kiislamu.
-
Iran na Nigeria kupanua ushirikiano wao katika uga wa nishati
Aug 27, 2022 20:52Waziri wa Mafuta wa Iran ameeleza matumaini yake ya kuimarika ushirikiano wa Jamhuri ya Kiislamu na Nigeria katika uga wa nishati.
-
Iran: Uhusiano wetu na Tanzania unazidi kustawi na kuimarika
Aug 27, 2022 07:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, uhusiano wa Tehran na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unazidi kuwa imara.
-
Iran inazalisha asilimia 98 ya dawa zake ndani ya nchi
Aug 27, 2022 06:47Shirika la Dawa na Chakula la Iran (FDA) limesema asilimia 98 ya dawa zilizoko nchini zinazalishwa na wataalamu wa taifa hili, na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ni miongoni mwa nchi 20 duniani zinazojizalishia dawa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
-
Makamu wa Rais wa Iran: Marekani na Ulaya hazina njia nyingine ghairi ya kukubali JCPOA
Aug 26, 2022 22:52Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na masuala ya uchumi amesema, vikwazo na mashinikizo ndiyo silaha ya mwisho kabisa ya Marekani na Ulaya na akaeleza kwamba katika hali ya sasa wao hawana njia nyingine isipokuwa kuyakubali mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran haitalegeza msimamo mbele ya adui
Aug 26, 2022 06:08Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia katu haitalegeza msimamo mbele ya adui ili taifa hili liondolewe vikwazo vya kidhalimu vya Marekani.
-
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran akutana na Rais wa Zanzibar
Aug 26, 2022 05:23Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu7 ya Iran aliyeko ziarani nchini Tanzania leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar na wawili hao wamesitizia udharura wa kuimarishwa ushirikiano baina ya pande mbili.
-
Kuundwa serikali ya wote, msimamo wa kiistratijia wa Iran kuhusu Afghanistan
Aug 26, 2022 03:06Mwaka mzima umepita tangu kuingia tena madarakani kundi la Taliban nchini Afghanistan, lakini hadi hizi sasa kundi hilo halijatambuliwa kimataifa kutokana na misimamo yake.
-
Iran yakosoa mkutano wa NPT kwa kutoshinikiza Israel ijiunge na mkataba huo
Aug 25, 2022 23:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameukosoa vikali Mkutano wa Kumi wa Kuangalia Upya Maazimio ya Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kuziia Uzalishaji na Usambazi za Silaha za Nyuklia NPT unaofanyika huko New York, kwa kukataa kutoa mwito kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kujiunga na mkataba huo wa kimataifa.
-
Jeshi la Iran laendeleza mazoezi ya ndege za kivita zisizo na rubani
Aug 25, 2022 03:35Mazoezi ya Pamoja ya Ndege Zisizo na Rubani (droni) 1401 ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameendelea kwa siku ya pili leo ambapo droni za kivita zimefanikiwa kutekeleza oparesheni zao kwa mafanikio.