Ghalibaf: Zana za ulinzi za Iran zimewatia kiwewe maadui; wanaogopa kuingia vitani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i87502-ghalibaf_zana_za_ulinzi_za_iran_zimewatia_kiwewe_maadui_wanaogopa_kuingia_vitani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, zana za ulinzi za Jamhuri ya Kiislamu zimeongeza nguvu za kujihami taifa hili, zimewatia kiwewe maadui na zimewafanya waogope kuingia vitani na Iran ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2022 20:53 UTC
  • Ghalibaf: Zana za ulinzi za Iran zimewatia kiwewe maadui; wanaogopa kuingia vitani

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, zana za ulinzi za Jamhuri ya Kiislamu zimeongeza nguvu za kujihami taifa hili, zimewatia kiwewe maadui na zimewafanya waogope kuingia vitani na Iran ya Kiislamu.

Mohammad Bagher Ghalibaf alisema hayo jana (Jumamosi) pembeni mwa maonyesho ya zana za ulinzi za Iran hapa Tehran na kuongeza kuwa mkakati wa Wizara ya Ulinzi ya Iran ni kuhakikisha taifa hili lina nguvu za kijeshi ambazo adui hawezi kufikiria kabisa kuanzisha vita dhidi yake. 

Vile vile amesema, stratijia ya kiulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuimaishara amani na utulivu na kuyahami mataifa ya wanyonge. Amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi na haina nia kabisa ya kuanzisha vita na nchi yoyote ile, lakini imesimama imara kujihami mbele ya shari na hujuma zozote na majibu yake huwa makali sana kwa adui.

Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Bunge la Iran

 

Aidha amesema, mafanikio ya taifa la Iran ya kujitosheleza katika uzalishaji wa zana za ulinzi yameleta heshima na ustawi pamoja na kujiamini kitaifa wananchi wa Iran, suala ambalo ni mafanikio makubwa sana katika kila upande.

Nguvu za kiulinzi za Iran hivi sasa ni kubwa kiasi kwamba leo Jamhuri ya Kiislamu inahesabiwa kuwa dola lenye nguvu kubwa zaidi za kiulinzi katika eneo hili. Ni dola la Kiislamu lenye ushawishi mkubwa kieneo na kimataifa na limefanikiwa kumtia kiwewe adui na kumlazimisha asifikirie kabisa kuanzisha vita dhidi ya yake.

Spika wa Bunge la Iran pia amesema, taifa hili limepata mafanikio hayo baada ya kuamini kuwa linaweza kujidhaminia lenyewe ulinzi wake. Nguvu za Jamhuri ya Kiislamu zinatokana kwa wananchi wenyewe ambao hivi sasa wamepata nguvu za kujiamini kitaifa kutokana na maendeleo ya kiulinzi ya nchi yao.