-
Kiongozi Muadhamu: Matukio ya dunia yanadhihirisha haja ya Iran na Russia kushirikiana zaidi
Jul 21, 2022 04:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo na Rais wa Russia hapa Tehran kwamba: matukio ya dunia yanadhihirisha kuwepo haja kwa Iran na Russia kushirikiana zaidi.
-
Rais wa Iran apongeza mapambano ya watu wa Syria
Jul 21, 2022 03:04Rais Ebrahim Raeisi wa Iran amesema ana yakini kuwa Syria ina mustakakbali mwema huku akiwapongeza wananchi wa Syria kwa mapambano na muqawama katika kipindi cha miaka 11 ya vita dhidi ya nchi hiyo ambavyo vinaungwa mkono na madola ya kigeni.
-
Amir-Abdollahian na Miqdad: Kuna ulazima wa kuheshimu mamlaka ya kujitawala Syria
Jul 20, 2022 23:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Feisal Miqdad wameshiriki katika kikao cha pamoja na waandishi habari na kusisitiza kuhusu kulindwa mamlaka ya kujitawala Syria.
-
Putin: Mazungumzo ya Marais wanaodhamini mchakato wa Astana yalikuwa ya manufaa
Jul 20, 2022 07:26Rais Vladmir Putin wa Russia amekitaja kikao cha viongozi wa nchi zinazodhamini mchakato wa Astana kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria kuwa muhimu sasna na kueleza kuwa kikao hicho kilikuwa na maudhui zenye manufaa.
-
Amir Abdullahian: Maadui wangali wanaendeleza njama mbovu ya kuibua migawanyiko na mifarakano
Jul 20, 2022 07:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe katika Mkutano wa Kwanza wa Kikanda wa Umoja wa Kiislamu na kusema: maadui wangali wanaendeleza njama mbovu ya kuibua migawanyiko na mifarakano.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu la kulindwa na kuheshimiwa umoja wa ardhi yote ya Syria
Jul 20, 2022 04:03Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kulindwa na kuheshimiwa umoja wa ardhi yote ya Syria na akasema: shambulio lolote la kijeshi linalofanywa kaskazini ya Syria, bila ya shaka litakuwa na madhara kwa Uturuki, Syria na eneo zima na litakuwa na manufaa kwa magaidi.
-
Taarifa ya mwisho ya mkutano wa Astana mjini Tehran: Hakuna suluhisho la kijeshi la mzozo wa Syria
Jul 20, 2022 02:25Katika taarifa ya mwisho ya kikao cha Astana mjini Tehran, Iran, Russia na Uturuki zimesisitiza kuwa, mzozo wa Syria hauna suluhisho la kijeshi na kueleza azma yao ya kuendeleza ushirikiano wa kupambana na ugaidi wa aina zote.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Wamarekani wanapaswa kufukuzwa kutoka eneo la mashariki mwa Furati huko Syria
Jul 19, 2022 22:57Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jioni ya jana (Jumanne) alifanya mazungmzo na Rais Vladmir Putin wa Russia na ujumbe aliofuatana nao hapa mjini Tehran, ambako amelitaja suala la Syria kuwa muhimu sana na kusema: Suala jingine muhimu katika kadhia ya Syria ni uvamizi wa Wamarekani na kukaliwa kwa mabavu ardhi zenye rutuba na zenye utajiri mkubwa wa mafuta za mashariki mwa Furati (Euphrates), na suala hili linapaswa kupatiwa ufumbuzi kwa kufukuzwa Wamarekani kwenye eneo hilo.
-
Kan'ani: Israe haina ubavu wala uthubutu wa kuikabili Iran kijeshi
Jul 19, 2022 21:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel hauna ubavu wala ujasiri wa kuingia katika makabiliano ya kijeshi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais wa Iran akutana na Putin na Erdogan na kujadili vita dhidi ya ugaidi
Jul 19, 2022 10:52Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi umepelekea kuimarika usalama katika eneo la Asia Magharibi.